*Thamani Yako Haipotei Bure.*
Mkulima mmoja alikuwa na ndoo mbili alizokuwa anatumia kutekea maji mtoni kisha kupeleka nyumbani.
Ndoo moja ilikuwa imetoboka kiasi cha kumwaga maji njiani na kufikisha maji nyumbani yakiwa yamepungua. Ndoo nyingine ilikuwa ni nzima na hivyo kufikisha maji yote nyumbani.
Baada ya siku nyingi kupita, ile ndoo iliyokuwa imetoboka ikahuzunika sana kwa kitendo kile cha kufikisha maji kidogo kila siku. Ikabidi ionyeshe huzuni hiyo kwa mkulima huyo.
Mkulima huyo akaishika mkono ndo hiyo na kuipitisha kwenye njia ambayo huwa anapita akiwa ametoka kuteka maji.
Pembeni mwa njia hiyo nyasi zilikuwa zimeota na kupendeza kiasi cha kuvutia sana macho. Ndipo mkulima akasema unahuzunika bure, huu uzuri wote unaouona ni kwa sababu ya wewe kumwaga maji njiani japo hutambue hilo.
*Jifunze kisha chukua hatua.*
[ ] Kuna vitu vya thamani unavifanya, huyaoni matokeo yake moja kwa moja lakini thamani yake ni kubwa sana.
[ ] Utaiona thamani ya kile unachokifanya kwa kujifanyia tathmini. Kila kazi unayoweka muda, nguvu na umakini hakiksha unajitathmini kujua thamani unayoipata na kile unachokikosa.
Dhana hii ya kutambua thamani ya hatua unazochukua ipo pia kwenye biashara yako ili kuweza kuimuza.
Kitabu cha *UWEZO WA KUANZISHA NA KUKUZA BIASHARA* imeeleza umuhimu wa kuipeleke biashara ysko Kliniki. Huku ni kufanyia biashara yako tathmini.
Jipatie kitabu hiki ili ujue maeneo sahihi ya kumwagilia kisha biashara yako kuchnua. Wasiliana: 0752 206 899.
Karibu sana.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz