Nguvu Kubwa Iliyojificha Kwenye Kuandika.
Haya ni maajabu ya akili yako! Je wajua kuwa ubongo wako una uwezo wa kuzalisha takribani mawazo 70,000/ kwa siku kwa kasi inayolinganishwa na kasi ya gari linalokimbia kuliko yote?
Kumbe tangu umezaliwa umewaza mawazo mengi sana! Lakini je unayakumbuka mawazo uliyowaza mwaka jana tarehe kama ya leo?
Kumbuka siku ile akili yako ilipopata wazo zuri sana na ukajiambia hili wazo lina thamani kubwa sana na kujiahidi utalifanyia kazi. Lakini baada ya muda wazo likayeyuka, ulijitahidi kulikumbuka lakini halikujia tena.
Kumbuka mwaka huu ulipokuwa unaanza. Ulikuwa na shauku kubwa ya kufanya makubwa sana. Uliwaza malengo mengi akilini mwako lakini mpaka leo kama siyo umeyasahau yote, basi unayakumbuka machache sana.
Hii ni ishara kuwa kuna kitu cha kufanya ili kuweza kunufaika na kazi kubwa inayofanywa na akili yako. Baada ya kupata wazo au ili kuweza kuboresha kwa kufikiri kwako nenda hatua muhimu inayofuata nayo ni KUANDIKA.
Zifutazo ni faida za kuandika mawazo yako.
- Unalifanya wazo kuwa wazi zaidi. Wakati wa kuandika, unaandika sentensi iliyo kamili
- Unaipunguzia akili mzigo. Badala ya kuifanya akili yako iendelee. kushikilia wazo jipya, liandike ili akili iendelee na mambo mengine.
- Unalipa wazo lako uelekeo wa kufanyiwa kazi. Kundika ni hatua ya kusogea kufanyia kazi wazo lako.
- Kurudia kuandika inasadia wazo hilo kukaa kwenye akili ya ndani kabisa kwa ajili ya kutafuta fursa za utekelezaji
Ndugu faidi hazina kubwa iliyopo kwenye ubongo wako kwa kuvuna mawazo yaliyo chanzo cha hatua yoyote kubwa unayotaka.
Hatua za kuchukua
- Kuwa na notebook ndogo ambayo unaweza kutembea nayo popote utakapokuwepo. Ukipata wazo jipya liandike haraka kabla halijayeyuka.
- Amka mapema kila siku andika ndoto, malengo na mipango ya maisha yako.
- Ipangilie siku yako kwa kuandika majukumu unayoyataka kuyatimiza hata kabla hujaianza siku hiyo.
- Unapokutana na changamoto, iandike kisha anza kufikiri na kuandika nini unaweza kufanya kuitatua changamoto hiyo. Utashangaa majibu mengi utakayoyapa.
Nguvu kubwa iliyolala kwenye fikra zako na jinsi ya kuiamsha kupata chochote unachotaka imeelezwa kiundani kwenye kitabu cha AMSHA UWEZO WAKO HALISI. Jipatie kitabu hiki ili uanze kufaidi nguvu hii mara moja. Piga 0752 206 899 kukipata sasa.
Karibu sana.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz