Kinachokuzuia Usiuone Mlango Wa Mafanikio Yako.
Ni dhahiri kuwa ili dreva aweze kuliendesha gari lake kisha kufika safari, hana budi kuijua barabara anayoiendea kwa usahihi kabisa.
Kadhalika ili uweze kufanikiwa katika maisha yako huna budi kujua mlango wa mafanikio ili uweze kupita huko na kukutana nayo.
Mlango wa mafaniko yako halisi ni kitu cha kipekee unachotakiwa kukifanya kwa upekee na kutoa thamani ya kipekee ambayo watu watakuwa tayari kukulipia kwa kiwango kikubwa.
Kitu cha kipekee cha kufanya huongozwa na ndoto yako kubwa.
Ndoto kubwa huogofya sana kiasi cha kukutisha mwenyewe.
HOFU ndiyo kimekuwa kikwazo kikubwa kwako kuuona mlango huo wa kukufikisha kwenye ukuu wako. Umeshindwa kutengeneza ndoto yako ya wazi kwa sababu mbele yako unaiona hofu na siyo mlango huo.
[ ] Kwa kuhofia kuwa wewe ni wa kawaida umeziba mlango wa mafaniko yako.
[ ] Hofu ya kuwa wewe huna bahati imeziba malango wa ndoto yako.
[ ] Hofu ya kuwa wewe huna uwezo wa kipekee(vipaji) imeziba mlango wa ndoto yako.
[ ] Hofu ya kuwa wewe hutaishi maisha marefu imeziba mlango wa ndoto yako.
[ ] Hofu ya watu watakuonaje imeziba mlango wa ndoto yako.
[ ] Hofu uliyoibeba ya watu walioshindwa imeziba mlango wa ndoto yako.
Umebeba hofu gani?
Njia kuu ya kuivuka hofu ili kuanza kuuona mlango wa mafanikio yako kupitia kujenga ndoto kubwa ni KUJIAMINI.
- Amini kuwa na wewe pia ni wa thamani kubwa na unastahili kupata mafanikio makubwa.
- Amini kuwa ndani yako kuna nguvu ya kipekee imelala tu ikisubiri uiamshe ufanye mambo makubwa.
- AMINI kuwa untakuwa na bahati kama utafanya maandalizi. Chukua hatua.
Kaa chini tafakari huku ukisikiliza moyo wako. Kama dunia ingekuwa na kila kitu cha kukuwezesha kupata chochote, ungependa upate nini, uwe nani, ufike wapi? Hii ni ndoto yako kuu; iandike na iweke wazi kisha anza kuiishi.
ANZA LEO ANZA SASA ANZA NA ULICHONACHO.
Kujua upekee ulionao ndani yako wa kukuwezeaha kufanya makubwa hapa duniani jipatie kitabu cha AMSHA UWEZO WAKO HALISI leo. Wasiliana: 0752 206 899.
Karibu sana.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz