Tembo Alitumia Hekima Siyo Ukubwa Wake. Jifunze Kwake….
Siku moja tembo alikuwa anataka kukatisha daraja ili kuvuka ng’ambo. Wakati akilisogelea lile daraja, alimuona nguruwe mchafu akiwa ndiyo anaanza kutembea kwenye lile daraja.
Baada ya kupiga hesabu za upana wa lile daraja, nguruwe aliona hawezi kukatisha lile daraja bila kugusana na yule nguruwe mchafu. Ndipo alipoamua kukaa pembeni akimpisha nguruwe akatishe kwanza.
Nguruwe alipita kwenye lile daraja na kumuona tembo akiwa amesimama pembeni. Baadaye ndipo tembo naye akaanza kukatisha lile daraja kuvuka ng’ambo nyingine.
Nguruwe alipoona haya aliwafuata wenzake huku akijisifu kuwa yeye ni mkubwa sana na wa kuheshimika kwa sababu hata tembo anamuogopa.
Baada ya kuona dhihaka hizo ndipo tembo wenzake walipomuuliza kwa nini yule tembo amefanya hivyo ili kuwadhalilisha?
Tembo yule akawajibu kuwa nilikuwa na uwezo wa kukatisha kwenye lile daraja muda huo na kumkanyagakanyaga yule nguruwe kwa miguu yangu tu, lakini sikufanya hivyo baada ya kuona nguruwe huyo ni mchafu na angeniambukiza uchafu wake.
Ona sasa hekika zangu zimenifanya niendelee kuwa msafi!
Jifunze;
Kuna mazingira yanahitaji hekima na si nguvu ili kulinda usafi wa mtazamo wako chanya ulionao. Mtazamo chanya ndiyo unaokufanya uchukue hatua sahihi, uvumilie kisha kupata kitu sahihi.
Lakini kuna mazingira unaingia kwenye mtego wa kuchafua fikra zako bila kujua au kujali.
Chukua hatua;
[ ] Acha mabishano yasiyo ya lazima ili usiambukizwe mtazamo hasi.
[ ] Angalia wanaokuzunguka hawakukatishi tamaa?
[ ] Uwe mwangalifu na mitandao ya kijamii taarifa nyingi ni za uongo, lakini unazibeba kama kweli!
[ ] Pisha kukaa bila kazi, unatoa nafasi ya akili yako kuwa karakana ya maovu.
[ ] Usiogope kusema HAPANA pale inapobidi. Usiwe wa kusema NDIYO kabla hujapima.
[ ] Fanya kilichosahihi bila kujali wengine watasema nini.
Kujenga mtazamo chanya na kuchukua hatua sahihi, jipatie kitabu cha DONDOO 366 ZA MAISHA YA MAFANIKIO ili usome DONDOO moja kila siku kwa mwaka mzima. Habari njema ni kuwa utatumia hata dakika tano tu kujua kilichosahihi kufanya, kuhamasika lakini kujua hatua sahihi ya kuchukua kila siku. Wasiliana nasi sasa kupitia 0752 206 899 kukipata kitabu sasa.
Karibu sana.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz