Hii Sasa Ndiyo Maana Halisi Ya Imani Ya Kupata Chochote.


Categories :

Kijiji kimoja kilikosa mvua kwa muda mrefu kiasi cha kusababisha ukame na njaa kali kijijini hapo. Ndipo walipoamua kukaa chini na kutafakari nini wafanye.

Baada ya kukaa chini na kutafakari kwa kina, wanakijiji hao walikubaliana kuwa wakutane siku moja wamuombe Mungu wao awape mvua.

Kwenye siku waliyopanga kukuatana kwa ajili ya maombi hayo, alionekana mtu mmjo aliyekuwa tofauti na watu wengine wote. Huyu alibeba mwavuli mkononi mwake.

Watu walimshangaa sana kwanini alikuwa amebeba mwavuli angali mvua hainyeshi kijijini hapo na hata hakukuwa na dalali zozote za jua kali!

Walimpomuuliza nini maana mambo hayo akasema, leo tumekuja kwa ajili ya kuomba Mungu atupe mvua. Nimebeba mwavuli huu ili kujifunika pindi mvua tuanayoiomba itakapoanza kunyesha.

“Imani halisi ni kukiona unachokitafuta ingali hakijitokeza kwenye uhalisia”

Chukua hatua:

  1. Kwenye ndoto yako kubwa uliyonayo, wewe endelea kuiamini kuifanyia kazi hata kama wengine wote watasema haiwezekani.
  2. Ukikutana na magumu kwenye safari yako ya mafanikio, iangalie picha yako ya mwisho, amini kuwa hivyo ugumu huo ndiyo unaoleta thamani za matokeo mzauri ya mwisho.
  3. Fufua leo mipango yako iliyokufa, ukiendelea kuiwekea kazi utapata matokeo mazuri.

Ndugu! Imani bila kazi haifai kabisa. Baada ya kuamini weka kazi. Hapa ndipo unapokuja umuhimu wa wewe kukipata kitabu cha JENGA NIDHAMU KALI.

Kitabu hiki kitakuwezesha kwenda hatua kwa hatua katika kujenga nidhamu kali kama tabia.
Hii ni nidhamu itakayokusaidia kujisukuma kuchukua hatua kubwa hata pale utakapokutana na ugumu au utakapokuwa hujisikii kuchuku hatua.

Kitabu hiki kitakujenga kwenye msingi wa kutoa MATOKEO na siyo SABABU. Wasiliana 0752 206 899 kisha jipatie nakala yako kwa bei ya ofa sh. 15,000/ badala ya sh 20,000/.

Karibu sana.

Imeandikwa na;

Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *