Tabia 12 Za Waliofanikiwa Sana(Sehemu ya Tatu).


Categories :

Kama kuna watu wanaofanikiwa sana huku wengine wakishindwa sana basi pia kutakuwa na kitu kinachowatofautisha sana hao waliofanikiwa na walioshindwa.

Kitu hicho ni TABIA. Waliofanikiwa wana vitu wanavyovifanya kila wakati kama sehemu yao ya maisha ambavyo ni tofauti na walioshindwa.

Baada ya kujifunza tabia nane za awali za waliofanikiwa kwenye makala mbili zilizopita, leo utajifunza tabia nyingine nne muhimu za waliofanikiwa kisha na wewe kuanza kuzijenga na kuziiishi;

  1. Wanajitofautisha.
    Kwa sababu ya ushindani mkubwa uliopo duniani, waliofanikiwa wanaamua kufanya vitu ambavyo watu wengine hawafanyi kabisa au wanafanya vinavyofanywa na watu wengine lakini kwa utofauti.
    Lakini walioshindwa wanaiga wanachofanya watu wengine na hivyo kukutana na ushindani mkubwa.
  2. Wanajiamini.
    Waliofanikiwa wanajiamini kwanza wao wenyewe kuwa wanaweza kufanya vile walivyopanga bila kujali ukubwa au utiishi wa hatua hizo. Hii inawapa fursa ya kuendelea kuweka nguvu kwenye mipango yao hata pale wanapokatishwa tamaa.
  3. Ni wauzaji bora.
    Waliofanikiwa wanaamini kuwa ili waweze kuuza kwa wengine thamani wanazozitengeneza wanahitaji kuwa na ushawishi mkubwa kwenye mauzo.
    Wanahakikisha wanaweza kuwaonyesha namna ambayo thamani wanayoitoa inaenda kutatua changamoto walizonazo na hivyo watu kushawishika kununua.
  4. Hawaogopi kushindwa.
    Moja ya changamoto kubwa inayowakumba walioshindwa ni kuogopa kushindwa. Hawachukui hatua ya kufanya vipya au kufanya makubwa kwa kuhofia kushindwa. Waliofanikiwa wanaikabili hofu kwa kufanya yale mazuri wanayoyahofia.

Chukua hatua:

  1. Kwenye biashara unayoifanya au kazi unayoifanya, angalia ni kwa namna gani unaweza kuanza kufanya kwa utofauti ili kuanza kupata matokeo ya tofauti. Je utawashukuru wateja kwa ujumbe saa chache baada ya kukutana nao? Je utafanya kwa ubora zaidi ya watu wengine?
  2. Orodhesha vitu ambavyo ungevifanya vingekupa mafanikio makubwa lakini hukuvifanya kwa sababu ya woga kisha jisukume kuchukua hatua ya kwanza ili hofu ife.
  3. Jipatie leo kitabu cha UWEZO WA KUANZISHA NA KUKUZA BIASHARA ili uweze kuanzisha na kukuza biashara yako na kuwa ya kipekee. Kupitia kitabu hiki utajua namna ya kujitofautisha kwenye biashara yako hivyo wateja kupata sababu ya kununua kwako na si kwa wengine.

Wasiliana kupitia 0752 206 899 ili kujipatia kitabu hiki sasa.

Kila la kheri.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *