Unawalea Nyoka Hawa! Watakumeza!
Ndiyo! Una nyoka ndani yako. Unaweza ikahamaki na kujiuliza kuwa nyoka gani unao ndani yako? Lakini kuna uwezekano mkubwa unao bila kujua.
Dada mmoja alikuwa na nyoka ndani yake aliyekuwa anamlea kama rafiki yake kwa muda mrefu tu. Lakini ilifika siku ambapo yule nyoka aligoma kula.
Licha ya dada huyo kumbembeleza nyoka huyo ale lakini hakufanikiwa. Ndipo alipoamua kumpeleka kwa daktari wa wanyama. Baada ya uchunguzi, daktari alimuuliza dada yule kama analala jirani na nyoka yule?
Dada yule akajibu ndiyo na analala naye karibu sana na usiku huteleza mwilini mwangu lakini hata nikimlisha chakula kwa sasa hataki kula.
Daktari yule akamuambia kuwa yule nyoka ana nia ya kumla yeye. Anakataa kule ili kupata nafasi ya kumuingiza yeye tumboni mwake. Lakini pia usiku huwa anateleza juu yake kaangalia unene wake ili kuja namna nzuri ya kummeza.
Daktari yule alimshauri dada yule kwenda kumuua nyoka yule kabla hajamdhuru.
Ndugu! Hata wewe kuna nyoka ambao umewafanya rafiki zako kwa muda mrefu sasa. Umewalisha na wanaendelea kukubembeleza huku wakiangalia namna ya kukumeza.
Hawa ndiyo nyoka ambao umewalea kwa muda mrefu sasa, wamekua na watakumeza.
- Maadui waliovaa uso wa urafiki. Kuna watu ambao wanaonekana kuwa ni marafiki lakini ni maadui. Hawa ni wale ambao hawapendi kabisa wewe ufanikiwe. Umeendelea kuwalea kwa kuwaambia kila kitu kuhusu maisha yako.
Chunguza vizuri nia za watu wako wa karibu na acha kushirikisha kila kitu kuhusu wewe. Weka mipaka.
- Mwili na uvivu wake. Umekuwa mzuri wa kupanga nini ufanye, lakini ukifanya kidogo tu mwili wako unakuambia umechoka. Una malengo mengi lakini matokeo kidogo..
Usiendelee kuubembeleza mwili wako kwani una asili ya uvivu. Usiukubalie kirahisi pale unapokuambia umechoka. Ukiendelea kuulea utameza mafanikio yako.
- Anasa.
Kil ukipata fedha unaendekeza starehe. Unaanda vizuri bajeti kabla hujapata fedha, lakini baada ya hapo unaendekeza starehe kiasi cha kutumia fedha ulizosema ni kwa ajili ya akiba na uwekezaji.
Kwa sababu unazilea anasa, zitameza kesho yako nzuri yenye mafanikio makubwa.
- Umasikini. Kutouchukia na kuukataa umasikini ni hatua za kuulea. Usiweke urafiki na umasikini hata kidogo. Kumbuka unapata kile unachokivumilia. Ukivumilia umasikini utaupata na kukumeza.
- Kuahirisha
Huyu ni nyoka ambaye amekuwa ukimlisha mara kwa mara. Unaweka mipango mizuri lakini muda wa utekelezaji ukifika, unasema utafanya baadaye au kesho. Nyoka huyu anazidi kukua na kama hutabadilika atakumeza.
Chukua hatua:
Rafiki! Ni nyoka gani umekuwa unamlisha kwa muda mrefu? Mtambue nyoka huyo au hao kisha anza kumuua sasa kwa kufanya tofauti na ulivyokuwa unafanya.
Kitabu cha JENGA NIDHAMU KALI ni mwongozo mzuri wa kukusaidia kuwaua nyoka hao kabisa. Huu ni mwongozo wa kukusaidia kubadili tabia zinazotaka kukumeza kisha kubaki hai na kukua kimafanikio.
Wasiliana kupitia 0752 206 899 kukipata kitabu hiki sasa kabla hujamezwa na nyoka hao.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz