Mambo Matano Ya kukupa Uthibiti Kamili Wa Maisha Yako.


Categories :

Ni raha iliyoje kama utafanikiwa kuchukua uthibiti kamili wa maisha yako! Pata picha hakuna kitu kinachokusumbua maishani mwako.

Naamini utajisikia vizuri ukifikia hali hii. Habari njema ni kuwa kuna uwezekano wa kufikia hali hii kama utafanikiwa kufanya au kuyapata mambo matano muhimu.  Mambo haya yamefupishwa na kuwa 5M.

1M ( Mouth) yaani mdomo
2M (Mind) yaani akili
3M (Mood) yaani hisia
4M (Manner) yaani tabia
5M (Money) yaani fedha

1M (Mouth); mdomo.

Kuna kiungo muhimu sana kwenye mdomo wako kinaitwa ulimu. Ukiacha ulimi kuhusika kwenye kula, hutumika sana kwenye kuongea.

Unaongea ni nini kina mchango mkubwa sana kwenye nini unafanya na kupata. Ulimi wako unaweza kutoa maneno ya kubomoa au kujenga. Yale unayoyaongea mara kwa mara ndiyo hushikwa sana na akili yako kisha kuamua nini upate.

Habari njema ni kuwa una nafasi ya kuchagua nini uongee. Tumia nafasi hii kujiongelea mema juu yako. Jiambie mimi naweza, mimi ni wa pekee, mimi ni tajiri …hakika yatakuwa yako.

2M (Mind); Akili.

Kuna kitu kimoja kimekaa juu ya mabega yako ni kitu kikubwa na cha ajabu sana kinachoweza kukupa chochote unachotaka.  Kitu hiki ni ubongo unaohusika kufikiri na kutoa mawazo.

Ndugu kumbuka kuwa kitu chochote hata utajiri huanza kama wazo. Akili yako kupitia ubongo huhusika katika hilo.

Kwa kutumia akili ndipo unapoweza kuamua nini unakitaka maishani mwako na kwa ukubwa gani.  Usijipunje! Unaweza kukipata kiasi chochote ambacho akili yako itaridhia. Patana na akili yakonini unataka, kiamini na kukifanyia kazi hicho.

3M (Mood); Hisia.

Kiwango cha kufanya kazi, kufurahia au kuchukia maisha hutegemea sana hisia unazokuwa nazo.

Kuna hisia chanya kama upendo, furaha, amani, shukrani, hamasa …. Lakini paia kuna hisia hasi kama chuki, hasira, kisasi, sonono, upweke….

Ili uapate uthibiti kamili wa maisha mwako kisha kufanikiwa kwenye M nyingine jizoweshwe kuwa na hisia chanya kila wakati na baadaye itakuwa tabia.

Kamwe usiache kila hisia ikuongoze kuwa kiongozi wa hisia zako; chagua chanya.

4M (Manner); Tabia..

Namna unayofanya vitu ndiyo inayoamua wewe ufanikiwe au ushindwe. Kufanya kitu kwa kujirudia rudia hutengeneza tabia.

Kuna tabia za mafanikio unazotakiwa kuzijenga. Nazo ni kutambua unachotaka, kuwajibika, kuweka malengo, kuweka kazi tena kubwa, kuweka akiba, kuwekeza, kutotumia zaidi kipato….anza kujenga tabia hizi sasa na utaweza kuthibiti maisha yako.

5M (Money); fedha.

Nadhani baada ya kusikia fedha akili yako imechangamka kuliko M nyingine.  Hii ni kwa sababu fedha ni mambo mengi. Ukiwa na fedha za kutosha unaweza kutatua changamoto nyingi zinazokukabili.

Kama kweli una nia ya kuwa na uthibiti kwenye maisha yako hakikisha lengo mojawapo kuu unalofanyia kazi ni kuwa tajiri.

Pata utajiri kwa kutoa thamani kubwa kwa watu wengine. Yaangalie matatizo yao kisha tumia uwezo wako kuyatatus na wao watakuwa radhi kukupa kiasi chochote cha fedha unachokitaka.

Ni M ipi kati ya hizi tano imekuwa ikikupatia changamoto kubwa sana kuijenga?

Habari njema ni kuwa kitabu cha AMSHA UWEZO WAKO HALISI ni mwongozo mzuri wa kufanikiwa kuwa na uthibiti wa M zote 5. Kuzitawala M hizo unahitaji nguvu na kitabu hiki kinakuonyesha nguvu kubwa ulizonazo kisha namna ya kuziamsha na kujenga utawala wako hapa duniani.

Jipatie nakala yako leo na anza na kuendelea kujenga uthibiti wa maisha yako.  Kitabu hiki kinapatikana kwa mfumo wa nakala nguvu(hard copy), tete(soft copy) na sauti(audio). Wasiliana kupitia 0752 206 899 kujipatia nakala yako sasa.

Karibu sana.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *