Jisukume Kuanzishaa Biashara Sasa.
UWEZO NA BIASHARA- 2
Jisukume Kuanzishaa Biashara Sasa.
Moja ya changamoto kubwa ya kujenga na kuikuza biashara ni kuanza. Watu wengi wamekuwa na nia ya kufanya biashara. Lakini ni muda mrefu sana tangu walipoongea na kupanga hivyo.
Miongoni mwa sababu kubwa iliyokufanga usianzishe biashara ni kuona kuwa hujawa tayari; ndiyo maana muda uliopanga kuanzisha ukifika unasema kesho.
Ili uweze kuivuka changamoto hii huna budi kuamua kuanza kuchukua hatua hata kama unaziona ndogo;
Anza kuandaa wazo.
Ukiwauliza watu kwa nini hawaanzishi biashara watakuambia ni kwa sababu hawana mtaji. Ukiwauliza je ikipewa mtaji utafanya biashara gani, atakuambia yoyote inayolipa.
Ndugu hakuna biashara moja inayomfaa kila mtu. Ili uweze kujenga biashara kubwa inatakayokupa mafanikio makubwa ni lazime ujenge biashara yako. Hii ni biashara inayotokana na kitu unachokipenda sana kufanya. Ni kitu gani upo tayari kufanya hata kama bure?
Anza kuweka mtaji.
Inawezekana una chanzo kingine cha kipato kama ajira au kibarua. Ili kuanza kupata mtaji wa kuanzisha biashara yako anza kutenga angalau 10% ya kila kipato. Weka nidhamu kubwa ya kuhakikisha unatenga kiasi hicho lakini pia kutokukitumia.
Anza kufanya utafiti wa soko.
Kwenye wazo la biashara unalofikiria, je nani atakuwa mteja wa bidhaa au huduma yako. Tengeneza mteja wa mfano. Kumbuka huyu ni mteja ambaye atakuwa na uhitaji wa bidhaa au huduma yako. Ni vizuri ukawa na uhakika wa soko hata kabla hujaanza biashara.
Anza kununua bidhaa kidogo kidogo.
Baada ya kujua biashara unayoweza kufanya na wateja unaweza kuwauzia, sasa unaweza kuanza kununua bidhaa kidogo kidogo na kuziweka. Hii itakupa hamasa kubwa ya kuanzisha biashara yako.
Anzia nyumbani.
Inawezekana umekuwa huanzishi biashara kwa sababu huna ofisi. Kwa zama hizo ambazo kuna maendeleo makubwa ya teknolojia na mawasiliano, unaweza kuwa na bidhaa chache nyumbani na kuanza kuziuza kwa njia ya mitandao au kuwafikia watu ana kwa ana. Hii itakupa hamasa ya kuendelea kufanya kwa ukubwa .
Anza kujifunza.
Kujifunza kuhusu biashara unayotaka kuijenga ni hitaji muhimu sana. Soma vitabu kuhusu biashara, hudhuria semina kuhusu biashara, Jitolee kufanya kazi kwenye biashara ya mtu.
Kwenye kila hali uliyopo kuna kitu unachoweza kuanza kufanya ili kufanikiwa kuanzisha na kukuza biashara ya ndoto yako.
Chukua Hatua.
- Angalia kitu unachokipenda sana kukifanya kisha ona ni kwa namna gani kitu unachopenda kukifanya kinaweza kutatua changamoto za watu. Pata wazo la biashara hapo.
- Anza kuweka angalau % ya kila kipato chako. Baada ya muda utakuwa na mtaji wa kuanzia biashara yako.
- Chunguza vizuri, kuna nafasi ya kuanza biashara yako yenye maono hata kwa udogo huo unaoudharau.
Anza LEO Anza SASA Anza na CHOCHOTE ulichonacho.
Kujifunza zaidi kihusu kuanzisha na kukuza biashara hakikisha umekipata kitabu hiki: UWEZO WA KUANZISHA NA KUKUZA BIASHARA. Kitabu hiki kitakuongiza namna ya kuanzisha na kukuza biashara ya ndoto yako hata kwa kuanza kwa udogo huku ukiwa na maono makubwa. Wasiliana kupitia 0752 206 899 kujipatia kitabu chako sasa.
Karibu sana.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz