Mheshimu Huyu Ukutane Na Mafanikio Yako.
Kwa sababu ya kiu kubwa ya kupata mafanikio, watu wametamani kupata matokeo wanayoyataka muda ya muda mfupi sana.
Kama ungekuwa unalinganisha na njaa ya chakula, watu wanatamani wapakue chakula na kula hata kabla hakijaiva.
MUDA ni kigezo kikubwa cha wewe kupata kile unachokita. Hata kama una haraka kiasi gani, ili uyapate mafanikio, mara nyingi unahitaji kuzipa jitihada zako muda.
Hii ni asili;
Hata kama mama mjamzito atakuwa amechoka na kutamani mtoto kiasi gani, hulazimika kuendelea kusubiri na kulea mimba kwa miezi yote tisa.
Hata kama una hamu kubwa ya kuiona kesho ili ulipwe deni ulilolisubiri siku nyingi, itakulazimu tu kusubiri masaa 24 yapite ili kesho hiyo ifike.
Hata kama una hamu kubwa ya kuuona mji unaouendea hata kama ni kwa ndege, itakulazimu uupe heshima muda ili ndege hiyo ipite umbali wote kati uliopo ili ikufikishe.
Ndugu najua umeweka mipango mizuri kwa ajili ya maisha ya mafanikio, lakini unaona kama unachelewa. Unatamani uyaone matokeo hayo sasa, lakini nakukumbusha kuwa kuna muda unaotakiwa upite ili matokeo hayo yaje.
Haraka zako zimekufanya kuanza kukata tamaa kwa kufikiria upo kwenye njia isiyo sahihi. Haraka zako zimekufanya uchukue njia za makato na zimekuumiza mno.
Chukua hatua.
- Weka mipango vizuri ya jambo ulilochagua kufanya; biashara, mahusiano, fedha, kazi,….
- Tambua jitihada/hatua unazotakiwa kuchukua ili kuweza kupata matokeo unayoyataka.
- Ainisha muda utakaochukua kwenye kila hatua ili kuweza kupata matokeo.
- Anza au endelea kuchukua hatua bila kuacha. Hata pale unapopata na changamoto na kuanguka, inuka tena kisha endelea na safari.
- Subiri matokeo huku ukiwa kwenye mwendo.
NB: Kama kuna jambo uliacha kuchukua hatua kwa sababu ya kutokuwa mvumilivu kwenye muda, lifufue sasa na kuendelea pale ulipoishia.
[ ] Ifufue biashara uliyoiacha kwa sababu ilichelewa kukupa faida.
[ ] Fufua uwekezaji uliouacha kwa sababu haukupa faida kubwa ndani ya muda mfupi.
[ ] Fufua utaratibu wako wa kuweka akiba. Ukiufanya kwa muda mrefu utakusanya utajiri.
[ ] Fufua ratiba yako ya kufanya mazoezi. Ukiyafanya kila siku afya yako itaimarika sana.
[ ] Fufua ratiba yako ya kuamka mapema. Ukifanya kwa muda mrefu utaona matunda ya kukamilisha malengo mengi.
Jipatie kitabu cha DONDOO 366 ZA MAISHA YA MAFANIKIO. Kitabu hiki kimeelezea kiundani kuhusu malengo, muda, kazi, thamani, ustahimilivu….ambazo ni nguzo muhimu sana kwenye kujenga mafanikio yako makubwa na ya kudumu. Wasiliana kupitia 0752 206 899 kujipatia kitabu hiki.
Karibu sana.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz