Kutikiswa Ndiyo Kukaa Sawa .
Baada ya kuweka mahindi kwenye gunia, hutikiswa kwa kulizungusha gunia na mzigo wake kushoto na kulia huku likinyanyliwa juu kidogo.
Kitendo hicho hufanya punje za mahindi kukujipanga vizuri. Lakini kuna nafasi juu ya gunia hupatikana baada ya kutikisa. Hii hutoa fursa ya kuongeza mahindi mengine kwenye gunia hilo.
Mitikisiko pia hutokea katika maisha yako. Pale unapojiona upo huru na kutulia, huibuka mambo ambayo hukutarajia kukutoa kwenye uhuru wako.
Watu wengi wamekuwa hawapendi mitikisiko. Hii ni kwa sababu inawatoa kwenye maeneo yao ya uhuru. Lakini ukiwa kwenye eneo la uhuru unakuwa huna mpango wowote wa kukua.
Kutikisika kwa kukosa sehemu ya kukopa fedha kwa ajili ya matumizi yako itakupa hamasa ya kujisukuma zaidi kukuza kipato zaidi.
Kutikisika kwa kutoelewana jambo moja na mtu wako wa karibu hutoa nafasi ya kurekebisha mambo mengine ambayo yalikuwa hayajaibuka.
Kutikisika kwa kuudhiwa na mtu kunatoa nafasi ya kujua hisia gani hasi bado hujaweza kuthibiti ili kuwa huru na matukio mabaya.
Ili uweze kukua unahitaji kutikiswa ili kujua udhaifu ulionao kisha kuweza kujijienga kisha kuwa bora zaidi.
Kila unapopanga kufanya makubwa tegemea kutikiswa. Ukiona unatikiswa basi tambua kuwa kuna kitu kipya unakifanya na hivyo unatakiwa kutumia vizuri fursa hiyo ya kutikiswa kukua.
Chukua hatua:
- Angalia viwango vyako kwenye maeneo mbalimbali maisha yako kama kipato, je unakua au bado upa palepale kwa muda mrefu?
- Weka malengo yatakayotikisa kiwango chako cha kipato. Kwa mfano weka lengo la kuanzisha biashara na hivyo kukuhitaji mtaji wa kuanzishia na kuendesha biashara hiyo.
- Pokea mtikisiko kwenye kipato chako kwa kuona sasa unahitaji kuweka nguvu kubwa kwenye vyanzo vya kipato chako ili kupata mtaji wa biashara hiyo.
- Kwenye kila eneo la maisha, baada ya kupata changamoto yoyote ile ona ni kwa namna gani unatumia nafasi inayopatikana baada ya mtikisiko kujiboresha zaidi.
Mtikisiko utakusaidia kujenga mafanikio kama utakubalia kuamsha nguvu ya ustahimilivu iliyopo ndani yako. Kuijua nguvu hii na nguzo nyingine 11 kama malengo, kazi, thamani, utajiri… za kujenga mafanikio ya kudumu, jipatie kitabu chako cha DONDOO 366 ZA MAISHA YA MAFANIKIO.
Wasiliana nasi kupitia 0752 206 899 ukipate kitabu hiki leo kwa bei ya ofa ili kujenga nguzo 12 za maisha ya mafanikio ya kudumu.
Karibu sana.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz