Epuka Kifungo Hiki Ili Uishi Kikamilifu…


Categories :

Maisha yako mwanadamu ni muda unaopewa uishi hapa duniani. Ni kipindi cha uhai wako ndipo unapoweza kufanya chochote unachotaka.  Baada ya kufa, hakuna historia mpya unayoweza kuitengeneza.

Lakini kumbuka kuwa maisha yako yamewekwa katika vipindi mbalimbali.  Kuna vipindi vigumu na rahisi, kulia na kucheka, kusogezwa na kutengwa, kukubaliwa na kukataliwa, kufanikiwa na kushindwa. Vipindi hivi vyote ni vyako.

Utafanikiwa kuishi maisha yako kikamilifu kama utatambua kila wakati kisha ukaishi wakati huo kikamilifu.

Kila wakati ni muhimu kwako kwani hata kama wakati huo utaonekana una sura mbaya lakini una maandalizi mazuri kwa ajili ya kukufanya uishi maisha yako kikamilifu.

Moja ya nyakati ambazo zimewapoteza wengi ni matukio ya nyuma ambayo hukuyatarajiwa na yakakushitua. Kwa sababu ya kuendelea kuyashikilia matukio hayo, umejibebesha mzigo mzito unaokuzuia kusonga mbele;

[  ] Umeendelea kuwalaamu waliokukosea badala ya kujikita kwenye malengo yako ya sasa.

[  ] Umeendelea kushikilia maumivu uliyoyapata kwenye kushindwa kwako badala ya kujifunza tu nini ukiboreshe kwenye kushindwa huko.

[  ] Umeendelea kushikilia hofu ya kushindwa kwa hatua iliyopita na sasa hutaki kujaribu vitu vipya.

[  ] Umeshikilia tabia ambayo haiwezi kukufikisha unakostahili. Je umesahau kuwa hakuna matokeo mapya utakayoyapata?

[  ] Umeendelea kung’ang’ania watu ambao walionekana marafiki lakini wamekuliza. Unasema umetoka nao mbali.

Ndugu! Nyakati zilizopita hazitakiwi kuwa mzigo kwako wa kukuzuia kuishi kikamilifu sasa na kujiandaa vizuri baadye.

Hakuna kitu chochote unachoweza kubadili kwenye kile kilichopita, kuendelea kushikilia maumivu hayo ni kujionea tu.

Usifungwe na kipindi chochote cha maisha yako. Kuwa huru ili uweze kuishi kikamifu na kufikia hatua ya mafanikio makubwa sana maishani mwako.

Chukua hatua;

  1. Usiyape uhai maumivu yako kasoro katika kujifunza.
  2. Kitumie vizuri kipindi cha sasa kwa kujisukuma kuchukua hatua za mipango yako bila ya kuahirisha.
  3. Usihofie sana kipindi kijacho, itumie leo kufanya maandalizi mazuri yako kesho yako bora.

Jipatie kitabu cha JENGA NIDHAMU KALI ili kuweza kuchukua hatua za malengo uliyoyapanga kwa kutokubali sababu yoyote inayoweza kukuzuia. Kwa kukipata kitabu hiki utatoa MATOKEO na siyo SABABU. Wahi nakala chache zilizobaki za bei ya ofa.

Kupata kitabu hiki cha JENGA NIDHAMU KALI tafadhali wasiliana kupitia namba 0752 206 899.

Karibu sana.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *