Hapo Ndipo Utaanza Kuishi…….
Baada ya kusoma kichwa hapo juu kuna swali litakuwa limekuja kichwani mwako mara moja, je ina maana sijaanza kuishi angali nimezaliwa siku nyingi zilizopita?
Kuna uwezekano mkubwa kuwa hujaanza kuishi licha ya kuwepo hapa duniani kwa muda mrefu. Kuna ukuta ambao upo mbele yako uliogawa maisha yako pande mbili.
Kuna uwezekano makubwa sasa upo upande mmoja wa maisha yasiyo halisi ukiacha maisha halisi upande mwingine. Ukuta unaotengeneza pande hizo mbili ni HOFU.
Huwezi kuishi maisha yako halisi kama utaruhusu hofu ndiyo uthibiti maisha yako. Kama umeshindwa kuikabili hofu, basi bado hujavuka upande mwingine wa maisha yako halisi.
[ ] Kama huweki mipango na kufanya makubwa kwa kuhofia kuwa huna uwezo, basi tambua hujavuka upande wa maisha yako halisi.
[ ] Kana kuna mambo unaogopa kufanya kwa hofu kuwa watu watakuchukuliaje, basi tambua kuwa bado hujavuka upande wa maisha yako halisi.
[ ] Kama hutumii ulichonacho kupata zaidi kwa hofu kuwa utapoteza ulichonacho, basi tambua bado hujavuka upande wa maisha yako halisi.
[ ] Kama unahofia kufanya vitu vipya kwa sababu utapata maumivu basi tambua hutaanza kuishi
Lakini kwa kuwa bado upo hai, una nafasi ya kuanza kusihi maisha yako halisi sasa. Vuka upande mwingine. Anza kwa kubadili mtazamo kuwa una maisha mengine halisi, makubwa na mazuri yanakusubiri.
[ ] Una nguvu kubwa ndani yako ambayo bado imelala tu. Usihofie utawezaje kufanya makubwa, mtaji unao ndani yako.
[ ] Kila mtu aliyopo duniani ana sababu maalumu ya uwepo wako. Umeletwa utatue tatizo fulani hapa duniani. Usihofu, una umuhimu mkubwa
[ ] Kila mtu huwa anaogopa lakini ni wale wanaojipa ujasiri wa kuikabili hofu, wanaanza kuishi.
[ ] Dunia ina utele, usiogope kujaribu kufanya makubwa, hata kama utapoteza utapata vingine.
[ ] Hofu ni kama barafu ambayo ukiiweka juani itasambaratika tu. Ukifanya unachohofia, hofu itakukimbia na utaanza kuishi maisha yako halisi.
Ndugu! Una nafasi ya kuanza kushi maisha yako halisi. Kuna mabadiliko makubwa utayapata utakapoanza kwenda zaidi ya pale ulipokuwa unaishia kwa ajili ya hofu.
Sasa anza kuweka malengo makubwa zaidi ukiamini una nguvu kubwa ndani yako, ambayo utakapoiamsha utafanikiwa kupiga hatua kubwa zaidi.
Kitabu cha AMSHA UWEZO WAKO HALISI kitakuwa msaada mkubwa wa kukuwezesha kuanza kuishi maisha yako halisi. Kupitia kitabu hiki utatambua wewe halisi na kuanza kumuishi huyo.
Jipatie nakala yako leo ili uache kuendelea kuigiza kuishi. Wasiliana kupitia 0752 206 899 kujipatia nakala yako sasa.
Karibu sana.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz