Yaache Mambo Haya Sita Upate Matokeo Ya Utofauti.
Kama kuna matokeo ya mafanikio umekuwa ukiyatafuta na huyapati basi kuna na mambo umekuwa ukiyafanya ambayo yanakupa matokeo usiyoyataka.
Njia pekee ya kuanza kupata matokeo tofauti na yale ni kuacha kufanya mambo hayo kisha kuanza kufanya tofauti na vile ulivyozoea.
Yafuatayo ni mambo ambayo ukiacha kuyafanya kisha ukaanza kufanya kinyume chake,lazima uanze kupata matokeo ya utofauti;
1. Toka kwenye eneo huru.
Kuna vitu ukivifanya havikufanyi usumbuke wala kufikiri zaidi. Hivi vinakupa raha. Umekuwa ukivifanya hivyo kwa muda mrefu sasa bila kupata matokeo ya utofauti.
Chukua hatua: Toka kwenye eneo huru kwa kuanza kufanya yale madogo ambayo umekuwa ukifanya sasa kwa ukubwa zaidi.
2. Kuahirisha.
Kila ukipanga hufanyi, ukiamini kuna muda mwingine wa kutosha kufanya hivyo. Hii ni saratani inayotafuta mafanikio yako.
Chukua hatua: Tafuta sababu kubwa ya kwa nini ukifanye ulichopanga. Jikumbushe mara kwa mara faida utakayopata kwa kuchukua hatua. Jisukume unaweza.
3. Raha za muda mfupi.
Mafanikio makubwa huchukua muda mrefu na huwa na maumivu makali. Ili kuukwepa muda mrefu na maumivu makali umekuwa ukikimbilia njia za makato.
Umeacha kuweka akiba ili uponde starehe za muda mfupi.
Chukua hatua:
Weka malengo makubwa kisha jitoe kuweka jitihada ili kuyafikia. Epuka njia za mkato kwani hazitakufikisha kwenye ukuu wako.
4. Mazingira hasi.
Epuka watu wanaosema huwezi, mazingira yanayokukatisha tamaa, habari zinazokuzimisha moyo. Hivi vyote vinasababisha usichukue hatua sahihi.
Chukua hatua;
Kuwa chanya kila wakati. Kuwa na watu sahihi wenye ndoto kubwa na wanokutia moyo kwenye safari yako. Pia epuka mazingira ambayo yatakuwa yanakupa habari hasi, mitandao ya kujamii, vyombo vya habari…
5. Usiogope kushindwa.
Woga ndiyo umasikini wako. Huwezi kupata matokeo ya utofauti na kufanikiwa bila kuchukua hatua za utofauti. Huwezi kuchukua hatua kama utakuwa na hofu ya kushindwa.
Chukua hatua.
Jipe ujasiri wa kufanya vitu vipya ili upate matokeo mapya. Kumbuka vingi unavyovihofia havitokei.
6. Muda huru.
Katika siku yako usiache muda wako bila ya kuupangia nini cha kufanya. Usipopanga nini ufanye basi utafanya chochote. Ni vigumu kupiga hatua kwa kuwa utaacha muda wako kupotea ovyo.
Chukua hatua.
Kabla hujaianza siku hakikisha unaipangilia vizuri na kukaa kwenye ratiba hiyo bila ya kuyumba.
Ndugu haya ni mambo sita ya kuacha na hatua sita za kuchukua ili kuanza kupata matokeo ya utofauti. Tafakari ni jambo lipi unaloweza kuliacha sasa kisha kuchukua hatua sahihi ili uanze kupata matokeo ya utofauti.
Kitabu cha JENGA NIDHAMU KALI ni mwongozo kamili wa kukusaidia kuacha mambo ambayo yamesababisha kushindwa kwako kisha kuwezesha kujisukuma kuchukua za mafanikio hata kama umechoka.
Kuna nakala chache zinazouzwa kwa bei ya ofa sh. 15,000/ badala ya sh 20,000/ zimebaki. Wasiliana kupitia 0752 206 899 kujipatia nakala yako sasa.
Karibu sana.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz