Toa Shingo Uone Mazuri Zaidi.
Kobe huwa anakuwa na machagua mawili. Ama afiche shingo yake kwenye nyumba yake na kubaki palepale au atoe shingo yake na kuona vitu vipya kisha kwenda mbele.
Asipotoa shingo yake maana yake ataendelea kubaki palepale kwani hataona njia ya kuiendea. Pia hakuna kitu kipya atakachoona zaidi ya kile kilichopo ndani ya nyumba yake. Mara nyingine ataona giza tu na kufikiri hakujakucha kumbe ni mchana.
Umemuiga kobe kuficha kichwa chake kwa kukaa eneo la faraja(comfort zone). Hujataka mahangaiko kwa kuendelea kufanya vitu vilevile hata kama havikupi matokeo ili mradi tu usisumbuke.
Lakini kumbuka huwezi kupiga hatua na kupata matokeo ya utofauti kama utaendelea kukaa kwenye eneo hilo la faraja.
Wanaopata matokeo ya utofauti ni wale wanoakuwa tayari kufanya vitu kwa utofauti huku wakijua vitahangaisha akili zao, vitawapa maumivu, watadharauliwa, wataonekana hawawezi…Lakini wanaamini hiyo ndiyo njia pekee ya kupata matokeo ya utofauti na makubwa.
Amua leo kuwa kobe anayetoa kichwa chake nje licha ya kuwa na hatari ya kukatwa, lakini ile aone vitu vipya na vizuri anaichukua hatari hiyo.
Chukua hatua;
- Usifiche kichwa chako kwa kuhofia kuishi maisha magumu baada ya kuanza kuweka akiba. Utaweza kuvumilia lakini itakuamsha kuweza kutafuta mbinu za kuongeza kipato zaidi.
- Toa kichwa kwa kuanzisha biashara. Usifiche kwa kusema utapata hasara, kama ikitokea basi tambua ndiyo njia ya kupata faida.
- Toa kichwa, weka ndoto kubwa sasa. Kumbuka hata ndoto ndogo zinakugharimu muda, nguvu, umakini…kwa nini usiwekeze rasilimali hizo kwenye ndoto kubwa!
- Toa shingo yako..nenda katafute nje ya duka lako. Kuna wateja nje wana uhitaji na bidhaa au huduma yako lakini hawaijui biashara yako.
- Toa kichwa chako. Soma vitabu kwani vitakupa maarifa mapya ya kufanya kwa utofauti. Kumbuka huwezi kufanya nje ya kile unachokifahamu. HABARI NJEMA💥. Ili kupata ujasiri wa kutoa kichwa nje kisha kuona uhalisia wa nguvu kubwa uliyonayo na mafanikio makubwa unayopaswa kuyapata, hakikisha unapata leo kitabu cha AMSHA UWEZO WAKO HALISI. Wasiliana kupitia 0752 206 899 kukipata kitabu hicho sasa. Kumbuka hii itakuwa hatua muhimu sana kwako kutoka nje ya gamba lako kuona ukuu ulionao katika dunia hii.
Karibu sana.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz