Wewe Anza Tu!


Categories :

Anza Leo….ni kauli ambayo nimekuwa nikiiandika mwanzo mwa dondoo ambazo naziandika kila siku.

Kauli hii nimekuwa nikiiandika baada ya kuona kuwa kitu kinachowatatiza watu wengi kutochukua hatua kisha kupata kile wanachokitaka ni kutovuka hatua ya kuanza.

Mtu anakuwa tayri ana malengo na mpango lakini haanzi. Mtu anakuwa na mtaji lakini haanzi biashara. Muda unafika lakini haanzi.

Ndipo nilipokuja na mpango huu wa kuanzisha kauli hii ya Anza Leo……. Lakini kauli hii nimekuwa nikiiendeleza kuwa Anza Leo, Anza Sasa, Anza na Chochote Ulichonacho.

Ndugu! Ukiangalia kiundani sana kuna matokeo mengi  umeshindwa kuyapata kwa sababu tu ya kutokuanza au kuchelewa kuanza.

Kuna mabadiliko makubwa sana yatatokea pale utakaamua kuanza kuchukua hatua kwa mipango unayoweka;

[  ] Anza na ulichonacho. Usisubiri uwe na kila kitu, angalia una nini, anza nacho. Hata kama ni mtaji mdogo anza nao. Hata kama itakulazimu kuanzia biashara nyumbani wewe anza tu.

[  ] Anza na wasiwasi ulionao. Kikwazo kikubwa cha watu kutokuanza huwa ni wasiwasi kama watapata matokeo yale wanayoyatarajia. Wewe anza, ukikosea utajifunza na kurudia ukiwa bora zaidi.

[  ] Anza na hofu uliyonayo. Njia pekee ya kuishinda hofu ni kufanya kile unachokiogopa. Unaogopa nini, anza sasa.

[  ] Anza hapo ulipo . Haijarishi hali uliyonayo sasa ya kipato, mahusiano, elimu, hisia…wewe anza.

[  ] Anza sasa. Hakuna muda mwingine wa kuanza zaidi ya sasa.

Kitu gani ambacho unaona ukikifanya kitaleta mabadiliko makubwa maishani mwako? Basi kianze kukifanya LEO, tena SASA  kwa kutumia CHOCHOTE ulichonacho.

Ili kuweza kuiishi nidhamu hii muhimu maishani mwako hakikisha unakipata kitabu cha JENGA NIDHAMU KALI.  Huu ni mwongozo wa kukufanya kuanza kupata matokeo.  Utaacha kutoa sababu kisha kuanza kutoa matokeo.

Wasiliana kupitia 0752 206 899 kujipatia kitabu chako sasa.

Karibu sana.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Kocha na Mwalimu(Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;
Simu; 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *