Mambo Ya Kuzingatia Ili Uweze Kukokotoa Faida Ya Biashara Yako.


Categories :

Je biashara yako inatengeneza faida? Wala sijui! Biashara nyingi zimekuwa zikiendeshwa bila kujua kama zinatengeneza faida au la! Kwa kutokujua hivyo watu wameendelea kufanya biashara miaka nenda miaka rudi lakini wakiona wapo paleple.

Biashara hukua pale inapokuwa na mzunguko chanya, yaani  fedha inayoingia kwenye biashara inapokuwa kubwa kuliko inayotoka. Ili uweze kuikuza biashara yako ni muhimu sana kuwa na uwezo wa kukokotoa faida ya biashara yako ambayo hutokana na mzunguko chanya wa biashara.

Kukukotoa faida imekuwa changamoto kwa watu wengi. Wafanyabiashara wengi hununua bidhaa, huuza , hutumia na kuendelea hivyo wakiamini kama wanauzo basi watakuwa wanapata faida bila kujali wametumia kiasi gani.

Yafuatayo ni mambo ya msingi ya kuzingatia kwenye biashara yako ili uweze kukokotoa faida au harasa kwenye biashara yako kisha kujua mwelekeo, kisha kuchukua hatua sahihi;

1. Mtaji unaozunguka.

Ni fedha kiasi gani unatumia kuzungushia biashara yako? Hii ni fedha inayotumika kununulia bidhaa au huduma. Hii haihusushi thamani ya samani, magari, nyumba nk. Kabla hujakokotoa faida, hakikisha huu mtaji wako upo kama taslimu, bidhaa au huduma.

2. Manunuzi.

Ili uweze kujua faida lazima kwanza utambue manunuzi uliyoyafanya. Hapa hakikisha kila bidhaa unajua umenunua kwa bei gani. Manunuzi yako.

3. Mauzo.

Kabla ya kuuza tambua ni faida gani unataka uipate. Faida ghafi ni tofauti ya bei ya kuuzia na kununulia. Faida ghafi lazima iwe kubwa ili pale utakapotoa gharama za uendeshaji basi faida kamili ipatikane.

4.Gharama za uendeshaji.

Hizi ni fedha zinazotumika kuendeshea biashara. Zinahusisha usafiri, bili mbalimbali, kodi mbalimbali, mishahara,. Hakikisha unaandika kila matumizi bila kujali udogo wake.

Eneo hili ndilo huwa chanzo kikubwa cha biashara kupata hasara. Hakikisha gharama za uendeshaji ni ndogo kuliko faida ghafi.

Sasa kokotoa faida.

Baada ya kujua mtaji wako unaozunguka, manunuzi, mauzo yako, gharama za uendeshaji; sasa unaweza kukokotoa faida  ya biashara yako.

  1. Faida ghafi:

Kumbuka hii siyo faida kamili, bali ni faida unayoipata kwa wewe kuuza bidhaa/huduma kwa bei kubwa kuliko iliyonunulia. Hii ni kabla ya kutoa gharama za uendeshaji.

Faida Ghafi = Jumla ya mauzo – Jumla manunuzi

Baada ya kupata faida ghafi sasa unaweza kukokotoa faida kamili.

Faida kamili = Faida ghafi –  ghrama za uendeshaji.

Huwezi kupata faida bila kuzingatia namba hizo hapo juu. Pia huwezi kujua kama biashara inakua kama hujui kama inazalisha fiada. Anza sasa kurekodi namba hizo hapo juu, kisha kokotoa faida kila siku, wiki, mwezi na mwaka.

Kitabu cha UWEZO WA KUANZISHA NA KUKUZA BIASHARA kina maarifa ambayo ni mwongozo mzuri wa kukusaida kuweka vizuri kila kumbukumbu ya biashara kisha kuweza kukokotoa faida.

Habari njema  ni kuwa leo utakipata kitabu hiki kwa bei ya ofa. Zimebaki nakala chache sana za ofa hii. Wahi na okoa sh 5,000/. Lipia saa sh 15,000/ badala ya sh 20,000/. Wasiliana nasi kupitia 0752 206 899.

Karibu sana.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwl. & Kocha (Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;Simu 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *