Hii Ndiyo Siri Ya Kuwa Mshindi Mbele Ya Changamoto Yoyote Ile.
Hakuna safari ya mafanikio isiyokuwa na changamoto. Kila ulipoweka malengo yako na kuamini matokeo yake yatakupeleka hatua nzuri zaidi, vikwazo vikaibuka na kukuzuia.
Hali ya kushindwa kwenye maisha yako ni kutokana na jinsi ulivyokubali kupigwa na changamoto ambazo zimekuwa zikisimama mbele ya jitihada zako.
Umejaribu kwa njia mbalimbali kujinasua, lakini kila ukitaka kuinuka, changamoto zimekudidimiza tena chini. Inawezekana umeshakata tamaa sasa na kuona wewe ni mtu wa kushindwa tu.
Habari njema ni kuwa kuna siri moja ambayo wanaitumia watu waliofanikiwa na kuwafanya wafanikiwe licha ya kukutana na changamoto kubwa kama unazokutana nazo wewe.
Siri hiyo unaweza na wewe kuitumia na kuanza kuwa mshindi pale unapokuwa upo kwenye ulingo na changamoto yako. Siri hii ni kuhakikisha changamoto inapopiga, wewe hupigwi.
Biashara inaweza kupigwa, mahusiano yanaweza kupigwa, mbinu zinaweza kupigwa, tarajio linaweza kupigwa, ……kamwe wewe usipigwe.
Kutokukubali kupigwa na changamoto ni;
[ ] Wewe kuwa mkubwa kuliko tatizo. Amini kuwa akili yako ina suluhu ya changamoto hiyo hata kama suluhu ya sasa hiajafanya kazi.
[ ] Kutoruhusu hofu ikutangulie. Vitu vingi unavyovihofia huwa havitokei. Ukihofia, unakubali changamoto ikupige kirahisi.
[ ] Kusimama baada ya kuanguka. Utaendelea na safari kisha kufika kama hata baada ya kuanguka utasimama tena na kuendelea na safari.
[ ] Kuvumilia pale matokeo yanapochelewa. Kuna matokeo yapo kwenye kile sahihi unachokifanya. Endelea kufanya matokeo yatakuja.
[ ] Utatumia muda kama dawa. Vidonda hupona kwa sababu muda umefika. Usiache kile unachofanya licha ya misukosuko, endelea ili muda wa kufa changamoto hiyo ukifika ukukute bado upo hai.
Anza kutumia mbinu hizi tano ili kuishi siri hii ya kutokukubali kupigwa na changamoto yoyote ile. Hapa ndipo utaanza kupata matokeo makubwa ambayo umekuwa ukiyakosa kwa sababu ya kukubali kupigwa na kila changamoto.
Japo kuwa, kuna kitabu cha AMSHA UWEZO WAKO kinachokupa mwongozo wa jinsi unavyoweza kuamsha uwezo wako uliolala ndani yako kisha kukabiliana na changamoto yoyote ile. Bado ni Tsh 15,000 tu, tuma ujumbe kwenda 0752 206 899. Zimebaki nakala chache tu za ofa.
“Unastahili Zaidi Ya Unachokipata”
Karibu sana.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwl. & Kocha (Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;Simu 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz