Fanya Hivi Ili Mteja Wako Aendelee Kununua.


Categories :

Hii ni hasara mojawapo umekuwa ukiitengeneza kwenye biashara yako.
Inawezekana umekuwa ukiitengeneza hasara hii bila kujua.

Biashara yako itauza sana kisha kukua kama mteja anayenunua mara ya kwanza anarudi kununua tena na kuendelea kununua katika kipindi chake chote uhitaji wake.

Sababu kubwa itakayomfanya mteja aendelee kununua kwenye biashara yako ni UBORA WA BIDHAA AU HUDUMA YAKO. Hata kama utakuwa na mahusiano mazuri naye, lakini kama bidhaa au huduma yako ni mbovu, atakukimbia tu.

Ni hasara kubwa kupata mteja kwa gharama kubwa kupitia masoko unayofanya, kisha mteja akanunua mara moja chache tu bila kurudi tena. Hii ni sawa na kuweka maji kwenye kikapu.

Fanya hivi ili kuwa na bidhaa au huduma bora itakayoendelea kumvutia mteja kuendelea kununua;

[  ] Jifunze kiundani juu ya bidhaa au huduma unayouza. Elewa bora ni ipi?
[  ] Ainisha sifa za ubora wa bidhaa unayoiuza kwa kuandika ili hata mtu mwingine kwenye timu anaweza kuipata.
[  ] Kama unatengeneza bidhaa mwenyewe, basi hakikisha umeshafanya majaribio kadhaa kisha kujua hatua za kufuata ili kupa bidhaa bora zaidi. Ziandike, zifuate na kila mtu anayehusika azifuate.
[  ] Kama ikitokea umepata au umetengeneza bidhaa mbovu, usiuze au waambie wateja wako kuhusu ubovu huo ili kama wataridhia wanunue angali wakijua. Hii itakuongezea imani kwa wateja wako.
[  ] Uwe na msimamo kwenye ubora wa bidhaa au huduma yako.
[  ] Jitofautishe kwenye ubora wa bidhaa ua huduma na wapinzani wako hata kama ni kwa kiasi kidogo sana. Wateja watafuata hicho.

Biashara yako itakuwa hai na kukua kama wateja wako wataendelea kuwa hai kwa kuendelea kununua kwako.  Ifanye bidhaa au huduma yako kuwa kivutio kikuu cha wateja kuendelea kununua. Anza kuzingatia mambo yaliyoorodheshwa hapo juu na biashara yako itakuua na kufikia mafanikio unayoyatarajia.

Endelea kujifunza zaidi kuhusu biashara na maendeleo binafsi. Tembelea tovuti yetu www.amshauwezo.co.tz. Huko utakutana na makala na dondoo zaidi ya 500 ambapo maarifa yake yataboresha mtazamo wako kisha kuchukua hatua sahihi.

“Unastahili Zaidi Ya Unachokipata Sasa”

Karibu sana.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwl. & Kocha (Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;Simu 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *