Kutana Na Mtu Huyu Aliyekukwamisha Kuwa Wewe Halisi. Mwambie Leo Aachane Na Maisha Yako.


Categories :

Kuna mafanikio umekuwa ukiyatamani au ulitakiwa kuwa nayo, lakini hujayapata kwa sababu kuna mtu amekuwa akikukwamisha.

Huyu ni mtu unayetakiwa kumpinga  na kutokuwa na urafiki naye kwa sababu ndiye aliyekufanya kuwa na hali uliyonayo sasa.

Mtu huyu amesababisha mambo haya maishani mwako;

[  ] Ulipokuwa unaweka malengo ndiye aliyekuambia wewe si mtu wa mambo makubwa, weka malengo madogo tu.

[  ] Ulipotaka kujisukuma kuchukua hatua ndiye aliyekuambia kwa nini ujitese!

[  ] Majibu ya jambo kubwa  yalipochelewa ndiye aliyesema uachane na unachofanya bali utafute njia za mkato bila kutambua kuwa ulikuwa unakaribia kuvuna matokeo makubwa.

[  ] Huyu ndiye aliyekudanganya wewe huna bahati, wale wanaofanikiwa wana bahati zao tangu kuzaliwa.

[  ] Huyu ndiye anayekushawishi uahirishe kufanya jambo muhimu sana leo, akikuambia utafanya kesho.

[  ] Huyu ndiye anayekuambia wewe huwezi kufanya biashara kwa sababu familia au kabila lako si wafanyabiashara wakubwa. Ndiyo maana bado unahangaika na kipato kidogo.

Kufupisha mambo, mtu huyu amekufanyia mengi ambayo sijayataja hapo lakini ndiyo yameleta maumivu makali maishani mwako.

Habari njema ni kuwa leo utamfahamu mtu huyo aliyekutesa kwa muda mrefu na kukufanya kutopata kile unachostahili.

Ili kumfahamu mtu huyo,  nenda pekeyako mbele ya kioo cha kujitazamia, je unamuona nani ndani ya kioo hicho? Huyo ndiye adui namba moja wa kushindwa kwako.

Mtu pekee aliyesababisha hali ya maisha uliyonayo ni wewe mwenyewe. Mapingamizi makubwa ya kukusababisha usikue yanaanzia ndani yako.

Hivyo kama unataka maisha mapya yenye matokeo unayostahili, huna budi kufanya mabadiliko makubwa sana ndani yako.

Mabadiliko makubwa unayotakiwa kufanya ili uweze kuchukua hatua za tofauti kisha kuanza kupata matokeo ya tofauti ni kubadili jinsi unavyovitazama na kuvichukulia vitu. Huku ni kubadili mtazamo wako.

[  ] Wewe ni mtu mwenye uwezo mkubwa wa kufanya makubwa. Uwezo huo umelala tu ndani yako.

[  ] Hakuna anayeweza kubadili chochote maishani mwako isipokuwa wewe mwenyewe.

[  ] Weka ndoto kubwa maishani mwako kwani muda unaotumia kuishi ndoto ndogo na kubwa ni sawa.

[  ] Baada ya kuwa na maarifa na ujuzi mzuri kinachofuata ni kazi. Weka kazi kubwa.

[  ] Utakutana na bahati maishani mwako pale fursa itakapokutana na maandalizi yako. Weka malengo kisha kazi. Bahati itakukuta njiani.

Ndugu! Uamuzi ni wako, kuendelea kuwa wewe wa zamani au kujitengeneza wewe mpya kwa kubadili mtazamo na kisha vitendo vyako.

Maarifa mapya na watu sahihi ni vyanzo vikuu vya kuwa wewe mpya na sahihi. Weka mpango wa kupata maarifa sahihi kwa kusoma vitabu.  Angalau kurasa kumi kila siku.

By the way kitabu cha AMSHA UWEZO WAKO HALISI kimewasaidia watu wengi kujiona wapya na kuanza kufanya kwa utofauti and ukubwa.

Baada ya kusoma kitabu hiki utatambua nguvu kubwa sana iliyolala ndani yako kisha kuanza kuiamsha na kuchukua hatua kubwa zaidi. Ukifanya kwa utofauti, matokeo ya tofauti ni lazima.

Jipatie kitabu chako leo ili uanze kubadili maisha yako leo. Wasiliana 0752 206 899.

“Unastahili Zaidi Ya Unachokipata Sasa”

Karibu sana.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwl. & Kocha (Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;Simu 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *