Je Na Wewe  Utakuwa Miongoni Mwa Watu Wataokuwa Wanajuta Kwa Sababu Hawakufanya Hivi….?


Categories :

 Mark Twain alisema “Twenty years from now you will be more disappointed by the things you didnot do than by the ones you did” ikiwa na tafsiri kuwa miaka ishirini kutoka sasa utakuwa utahuzunishwa na vitu ambavyo hukufanya kuliko vile ulivyofanya.

Kabla hujafikiri miaka 20 ijayo, fikiri miaka 20 iliyopita; kuna vitu ambavyo vinakuumiza kwa kutovifanya, tena kuliko vile uliyovifanya.

Kadhalika miaka 20 iyayo kuna vitu vitakuwa vinakuumiza kwa sababu utakuwa hujavifanya kuliko vile utakavyokuwa umevifanya.

[  ] Utaumia kwa sababu hukuutambua upekee wako na kuuishi bali uliiga maisha ya mtu mwingine. Hivyo umekuwa mtu wa kawaida sana.

[  ] Utaumia kwa sababu kulikuwa kuna fursa kubwa ya kuifanya na kupata mafanikio makubwa lakini hukufanya kwa sababu ya hofu. Na sasa fursa hiyo imeshayeyuka.

[  ] Utaumia kwa sababu kuna biashara hukuanza kwa kuona muda bado. Hivyo utakuwa kwenye mahangaiko ya kipato.

[  ] Utaumia kwa sababu kila fedha uliyoipata mikononi mwako uliitumia yote bila kuweka akiba na hivyo unaendelea kuwa mtumwa wa fedha.

[  ] Utaumia kwa sababu ya kuna marafiki ambao ulitakiwa kuachana nao lakini wewe ukakomaa nao kisha wamekushikilia ubakie wa kawaida kama wao.

[  ] Utaumia kwa sababu utakuwa hujafanya uwekezaji wowote huku wenzako uliowacheka wakati wanawekeza sasa wanavuna faida kubwa…na muda utakuwa umekwenda.

Ndugu! Kama sasa unajuta kwa sababu ya miaka 20 iliyopita sema inatosha na sikubali tena kuumia kwa miaka mingine 20 ijayo.

Kaa chini kisha tafakari nini hasa unakitaka maishani mwako. Orodhesha vitu vyote na baada ya hapo ainisha kitu kikubwa ambacho unaona ukikianza kitabadilisha maeneo mengi maishani mwako. Kisha anza leo, anza sasa na anza na ulichonacho.

Je ni kuanza biashara? Je kuanza uwekezaji? Je ni kuanzisha kampuni? Je ni kukuza kipaji chako?

Sasa acha woga, jipe ujasiri wa kuanza na endelea kujiboresha kila siku.

By the way kitabu cha JENGA NIDHAMU KALI kitakuwa msaada mkubwa sana kwako katika kufanya maamuzi haya makubwa.

Kitabu hiki kitakupa mwongozo wa kutengeneza KWA NINI KUBWA ya kukufanya kuchukua hatua ngumu ambazo umekuwa uzikimbia au kuziahirisha mara kwa mara. Hivyo utaanza kupata matokeo ambayo umeyasubiri kwa siku nyingi.

Wasiliana kupitia 0752 206 899 kukipata kitabu chako sasa. Usitengeneze mazingira ya kuja kujuta tena.  Kipate kitabu hiki sasa.

“Unastahili Zaidi Ya Unachokipata Sasa”

Karibu sana.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwl. & Kocha (Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;Simu 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *