Hii Ndiyo Siri Kuu Wanayotumia Mashujaa Kushinda. Anza Kuitumia Leo Kuwa Shujaa Wa Maisha Yako.


Categories :

Unapoambiwa huyu mtu ni shuajaa picha ya haraka inayokuja akilini  mwako ni kumuona mtu huyo alikuwa kwenye vita na ameshinda vita.

[  ] Alikutana ana adui akamshinda.
[  ] Alikutana na mazingira ya kuogofya lakini akasonga mbele, hakurudi nyuma.
[  ] Wengine walipomwambia arudi nyuma alikataa na kusonga mbele.
[  ] Hata pale kila mtu aliporudi nyuma, yeye aliendelea.
[  ] Hata pale matokeo ya jambo  analolipigania  yalipochelewa aliendelea kwa imani kuwa matokeo yatatokea mbeleni.
[  ] Hata pale alipoona hili jambo lina hatari ya kumpa kifo, lakini aliendelea tu.

Ukiangalia sifa hizi za shujaa utagundua kuwa si kwamba shujaa huwa hashindwi la hasha! Inawezekana anashindwa kama unavyoshindwa wewe. Na kuna uwezekano mkubwa kuwa anashindwa kuliko wewe.

Kumbe ni nini basi mashujaa wanaibuka washindi angali wakikabiliwa na changamoto lukuki?  Kuna siri ya wao kuwa washindi ambayo unaweza kuitumia katika maisha yako na kuwa mshindi kwenye malengo uliyonayo.

Siri hii imeainishwa vema kwenye kauli aliyoitoa Confucius; “A man is great not because he has failed; a man is great because failure hasn’t stopped him.” ikiwa na tafsiri kuwa mtu ni mkubwa kwa sababu hajashindwa, bali mtu anakuwa mkubwa kwa hajaruhusu kushindwa kumsimamisha kwenye kile anachofanya.

Kumbe siri ya kuwa shujaa ni kutoruhusu kushindwa kuwa kikwazo cha kutopata kile unachotaka.

Licha ya kuwa na malengo na mipango mizuri ya kupata kile unachokitaka, bado utakutana na changamoto nyingi zitakazokukwamisha  na kukufanya kushindwa. Lakini kumbuka jambo moja ambalo na mashujaa hukumbuka. Kushindwa si mwisho wa mapigano…endelea.

Dunia itataka kukupima kwa kila aina .ya mitihani ili kutambua kuwa kama kweli una nia ya kukipata kile unachokitaka. Unahitaji kushinda mitihani hiyo kwa kutokubali kukata tamaa.

Chukua Hatua Leo:

  1. Tafakari juu ya malengo yenye thamani kubwa  uliyoanza kuyafanya lakini uliacha kwa sababu ulishindwa mara kadhaa. Tumia siri hii uliyojifunza. Kafufue. Jifunze kwenye makosa uliyofanya kisha endelea mpaka umepata matokeo.
  2. Weka mipango yako mipya ya chochote unachokitaka.  Jiambie kuwa lazima niwe shujaa kwenye malengo haya kwani sitakubali kukatizwa na kushindwa kwangu. Nikishindwa, nitajifunza na kurudi nikiwa bora zaidi.

Ushujaa kwenye maisha yako utatengenezwa na wewe mwenyewe. Anza leo kuutengeneza.

“Unastahili Zaidi Ya Unachokipata Sasa”

Karibu sana.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwl. & Kocha (Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;Simu 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *