Huyu Ndiye Adui Mkuu Aliyezuia Mafanikio Yako Kwa Muda Mrefu. Usikubali Kuendelea Kuwa Mnyonge Kwake…


Categories :

Kuna adui mmoja ambaye ameua ndoto kubwa ulizokuwanazo.

Adui huyo amekufanya kushindwa kutimiza malengo uliyojiwekea mwaka huu.

Adui huyo anakufanya usijaribu vitu vipya ambavyo vingekufanya ukue.

Adui huyo anakufanya usianzishe biashara akikwambia utapoteza fedha yako.

Adui huyo anakufanya usikutane na watu wakubwa na muhimu ambao wangekufanya upige hatua.

Adui huyo amekufanya usiendelee kuchukua hatua baada ya kushindwa mara moja tu.

Hali yako mbaya ya kifedha, mahusiano, afya, binafsi na kiroho imechangiwa sana na wewe kumruhusu adui huyu kusimama mbele yako.

Adui huyo aliyekutesa kwa muda mrefu ni HOFU na hasa hofu ya kushindwa.

Umeiruhusu hofu itawale na imekukwamisha kweli kweli. Hakuna kitakachobadilika bila kumkabili huyu adui na kumtawala.

Kumbuka ulipokuwa mtoto hukuogopa chochote hivyo umejifunza kuwa na hofu.

Hofu ni kitu cha kufikirika ndiyo maana huwezi ukaishika mkononi. Hivyo utaishinda hofu kwa kuanza kubadili mtazamo wako tu.

Kuanzia sasa, hofu inapotaka kusimama mbele yako na kukukwamisha kumbuka haya kisha vaa ujasiri wa kufanya kile muhimu unachokiogopa na kupata matokeo makubwa unayostahili.

[  ] Kila mtu ana hofu, wewe kuwa miongoni mwa washindi wa wanaoisogolea hofu.

[  ] Vitu vingi unavyoviogopa havitokei na hata vikitokea siyo kwa ukubwa ambao wewe unaukuza.

[  ] Njia pekee ya kuishinda hofu ni kufanya kile unachokiogopa.

[  ] Hofu ni kama barafu,  ukiliweka juani litayeyuka. Hivyo hofu huyeyuka pale unapoendelea kufanya kile unachokiogopa.

[  ] Mafanikio yako makubwa unayostahili yapo mbele ya kile unachokiogopa.

Kama kuna jambo moja ambalo litaboresha maisha yako kabisa, ni kufanikiwa kuitawala hofu yako.

Utafanikiwa kuitawala hofu yako kwa kuamsha nguvu ya kujisukuma ili kuchukua hatua hata pale unapohofia.

By the way kitabu cha JENGA NIDHAMU KALI kimekuwa msaada kwa watu wengi kujisukuma kuchukua hatua zile wanazozihofia kwa kanuni ya kuainisha KWA NINI KUBWA.

Hii ni kanuni ya kutambua sababu kubwa inayokupa ujasiri unaozishinda hofu zozote zile.

Jipatie kitabu hiki leo kwa ofa ya Mwaka mpya ili uweze kufanya maandalizi ya kupata matokeo makubwa mwaka 2024. Wasiliana nasi kupitia 0752 206 899.

“Unastahili Zaidi Ya Unachokipata Sasa”

Karibu sana.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwl. & Kocha (Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;Simu 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *