Wafahamu Maadui Hawa Sita Watakaokula Muda Wako Kisha Kukufelisha Mwaka 2024…
Kama kuna rasilimali muhimu sana ya kukufanya ufanikiwe mwaka 2024 basi ni muda.
Lakini kuna maadui sita waliojipanga kuhakikisha wanaiba muda wako. Wafahamu leo ili ufanikiwe kuwathibiti wasikukwamishe..
1. Kuahirisha….
Jisukume kuchukua hatua kila unapopanga, kuahirisha ni kutakupotezea muda na kuchelewesha maendeleo yako.
2. TV, Simu & Mitandao ya kijamii.
Hivi ni vitu vyenye uraibu mkubwa sana enzi hizi. Punguza matumizi ya vitu hivi kwa kiasi kikubwa uwezavyo. Itumie simu yako kwa kiasi kikubwa pale inapokuwa kama ofisi yako.
3. NDIYO….
Ukiwa mwepesi wa kusema ndiyo kwenye kila jambo uwe na uhakika kuwa utakosa muda wa kufanya mambo yako ya msingi. Weka ratiba yako na baada ya hapo sema hapana kwenye mambo mengine.
4. Kufanya vitu vingi kwa pamoja.
Je unaamini kuwa uzalishaji utaongezeka kwa kufanya vitu vingi kwa pamoja? Hapana. Hii kupoteza sana muda wako….shika jambo moja lifanye mpaka mwisho kisha hamia jingine.
5. ‘Bado sijawa vizuri’….
Huyu ndiye adui aliyechelewesha mafanikio yako kwa kiasi kikubwa. Kila wakati umesema bado hujajiandaa vizuri…miaka imepita sasa…Usiendelee kupoteza muda tena anza na ulichonacho, anza sasa.
6. Hofu.
Mwaka 2023; Kuna vitu umeshindwa kuvianzisha kwa sababu ya hofu. Kuna watu muhimu hukuonana nao kwa sababu ya hofu. Hukufanya nje ya mazoea kwa sababu ya hofu…..mwaka huu weka hofu pembeni inakupotezea muda kwa sababu vitu vingi unavyovihofia havipo kwenye uhalisia, vipo kwenye akili yako tu..
Ili mwaku uwe wa mafanikio makubwa kwako, hakikisha unawashinda maadui hawa.
Ili uweze kuwashinda maadui hawa, huna budi kujenga nidhamu kali. Hii ni nguvu ya kujisukuma kuchukua hatua sahihi bila kuruhusu sababu yoyote ile.
Hata hivyo kitabu cha JENGA NIDHAMU KALI ni mwongozo kamili wa kukusaidia kujenga nidhamu kali itakayokuwezesha mwaka 2024 kuwa wa kutoa matokeo na siyo sababu.
Habari njema ni kuwa utakipata kitabu hiki leo kwa bei ya ofa ya mwaka mpya. Wasiliana kupitia 0752 206 899 kuwahi nakala chache za ofa zilizobaki.
“Unastahili Zaidi Ya Unachokipata Sasa”
Karibu sana.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwl. & Kocha (Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;Simu 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz