Tambua Na Ishi  Siri Hii Ya Kufikia Mafanikio Yako Makubwa.


Categories :

Kama kuna mtu amekuambia kuwa waliofanikiwa hawashindwi basi  amekudanganya.

Ukweli ni kuwa waliofanikiwa ndiyo waliojaribu na kushindwa mara nyingi kuliko walioshindwa.

Siri kubwa ya waliofanikiwa kushinda kwao imejificha kwenye ukweli kuwa waliofanikiwa hawaachi kuendelea kuchukua hatua hata baada ya kushindwa kwao.

Naamini na wewe kuna kitu kimoja kikubwa unatamani kukipata maishani mwako. Iishi siri hii; Endelea kukifanya kitu hicho hata baada ya kushindwa.

Yaishi mambo haya 10 ili kunufaika na siri hii kubwa ya mafanikio yako makubwa.

  1. Weka lengo lako kubwa licha ya hofu ya kushindwa.
  2. Ukishindwa jifunze ulipokosea kisha rudi ukiwa bora zaidi.
  3. Usikae muda mrefu sana ukisubiria kuanza kufanya tena. Utazidi kupotea.
  4. Usiamini kuwa na wewe huwezi kwa sababu kun wengi walioshindwa. Ungana na wachache walioshinda.
  5. Tambua kuwa kushindwa si kosa bali ni kutokujua njia sahihi ya kukifanya kitu hicho.
  6. Kumbuka kushindwa kutakuwa ni kuchelewa tu kufika mwisho mzuri kama utaamuka baada ya kuanguka.
  7. Tambua kuwa waliofanikiwa ndiyo waliojaribu mara nyingi na kushindwa   kuliko walioshindwa.
  8. Usijilaumu kutokana na kushindwa kwako bali jifunze kutokana na kushindwa kwako.
  9. Ukitaka upate mafanikio makubwa basi jaribu na kushindwa mambo makubwa.
  10. Wewe usipokubali kushindwa hakuna mtu wa kukuzuia kupata unachokitaka.

Je unataka kufanikiwa haraka? Kama jibu ni ndiyo basi ongeza kasi ya kushindwa na kuinuka.

Lakini ili uweze kuendelea kuchukua hatua baada ya kushindwa, huna budi kuamsha nguvu ya kujisukuma kuchukua hatua hata kama hujisikii. Jambo hili huwa changamoto kwa watu wengi.

Habari njema ni kuwa kitabu cha JENGA NIDHAMU KALI ni mwongozo wa kukuwezesha kuamsha nguvu ya kujisukuma ili kuendelea kuchukua hatua hata kama unakutana na magumu.

Kuna nakala chache za ofa ya mwaka mpya zimabaki. Walisiliana nasi kupitia 0752 206 899 ili kujipatia nakala yako sasa.

“Unastahili Zaidi Ya Unachokipata Sasa”

Karibu sana.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwl. & Kocha (Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;Simu 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *