Zifahamu Njia Tano Za Kupata Wazo La Biashara Sahihi Kwako.  Hizi Mbili Ni Muhimu Zaidi..


Categories :

Biashara nyingi hufa kwa sababu ya kutozingatia hatua muhimu ya kwanza ya kaunzisha biashara.

Hatua hiyo muhimu ni kupata wazo sahihi la biashara yako.

Wazo la biashara yako lazima liguse maumivu au matamanio waliyonayo wateja wako.

Watu kuanzisha biashara kisha kuanza kutafuta wateja.  Ndipo huja kugundua kuwa watu wachache sana wana uhitaji na bidhaa au huduma ya biashara yako.

Nitapataje wazo la biashara? Vigezo gani nitumie ili kupata wazo bora la biashara yangu?

  1. Uliza familia yako au rafiki zako. Hawa ni watu wako wa karibu wanoweza kukuambia ni mahitaji gani wanayatafuta na hawajayapata au hata kama wameyapata lakini hawajaridhika. Hii itakuwa ni fursa kwako kujua watu wanahitaji nini.
  2. Ainisha changamoto unazokutana nazo na zitatue. Kwa kuainisha changamoto unazokutana nao kila siku na kuzitafutia majibu utapata wazo la kuona ni kwa namna gani unaweza kutatua changamoto unazokutana nazo wewe kwa watu wengine.
  3. Vitu unavyovipenda. Vitu gani unapenda kuvifuatilia na kuvifanya  kama ‘hobi’ zako? Je vitu hivyo haviwezi kuwa na thamani kwa watu wengine? Kwa mfano kama una- hobi ya kufutilia mpira kwa nini usianzishe sehemu ya kuangalia mpira na watu wakakulipa?
  4. Vitu gani unavifanya kwa ukubwa na kwa urahisi? Huko ndiko kwenye kipaji chako. Mafanikio makubwa yapo kwenye kipaji chako.
    Kama kipaji chako ni kufundisha,  anza hata kwa kuwafundisha watoto nyumbani kisha fungua kituo cha ‘tution’ na baadaye shule.
  5. Angalia biashara zilizopo.
    [  ] Biashara zilizopo zinaweza zikawa hazipo maeneo mengine. Kaanzishe huko.
    [  ] Biashara zilizopo zinaweza zikawa na mapungufu, azisha kama hiyo lakini wewe boresha mapungufu hayo na jitofautishe.

Tumia njia hizi kupata wazo la biashara unayoweza kuianzisha.

Njia(vigezo) hizi mbili ni muhimu zaidi  kuzingatia ili kuanzisha na kukuza biashara yenye mafanikio ni.

  1. Biashara yako itokane na changamoto kubwa zinaowakabili watu kila siku.
  2. Uwe na mapenzi na biashara unayotaka kuifanya. Hii itakufanya udumu hata utakapokutana na changamoto.

Biashara gani unaweza kuianzisha au kuiboresha?

Hata hivyo kujifunza na zaidi kuhusu kuanzisha na kukuza biashara hakikisha unajipatia kitabu chako cha UWEZO WA KUANZISHA NA KUKUZA BIASHARA.

Kitabu hiki kitakuongoza hatua kwa hatua kuanzisha na kukuza biashara yako kisha kufikia mafanikio makubwa. 

Habari njema ni kuwa una nafasi ya kupata nakala chache zilizobaki zenye bei ya ofa. Wasiliana nasi sasa kupitia 0752 206 899 kujipatia nakala yako.

“Unastahili Zaidi Ya Unachokipata Sasa”

Karibu sana.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwl. & Kocha (Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;Simu 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *