Fahamu Wakati Sahihi Wa Kutengeneza Faida Kwenye Biashara Yako.
Kama unasema una biashara halafu haitengenezi faida, basi tambua huna biashara.
Mhimili mkuu wa biashara yoyote ile ni FAIDA na si vinginevyo.
Je wakati sahihi wa kutengeneza faida ni upi? Je ni wakati wa mauzo? Je ni wakati wa matumizi? ….
Wakati sahihi wa kutengeneza faida ya biashara yako ni wakati wa manunuzi au uzalishaji.
Bidhaa au huduma unayouza unaweza kuinunua ikiwa tayari kwa kuuza au unaweza kutengeneza mwenyewe kutoka kwenye malighafi mbalimbali.
Wakati wa kununua bidhaa iliyokamilika au kutengeneza bidhaa yako mwenyewe, ndiyo wakati sahihi wa kutengeneza faida ya biashara yako.
Faida ya biashara yako uanze kuiona mapema tu unapopata bidhaa au huduma ya kuuza.
Hivi ndivyo unavyoweza kutengeneza faida wakati wa kununua au kuzalisha bidhaa au huduma;
[ ] Tengeneza au nunua bidhaa au huduma inayohitajika na watu. Usinunue kwa sababu inakupendeza wewe tu.
[ ] Tengeneza au nunua bidhaa bora ambayo itatakuwa rahisi kuuzika.
[ ] Nunua bidhaa bora kwa bei ya chini au punguzo. Fanya utafiti kujua ni wapi unaweza kupata.
[ ] Nunua au zalisha kwa wingi ili kupunguza gharama.
[ ] Panga kabisa mapema bei ya kuuzia bidhaa au huduma yako kabla ya kuiweka sokoni.
[ ] Unapoiamini bidhaa au huduma yako kuwa ina thamani kubwa, usisite kupanga bei kubwa licha ya kununua kwa bei ya chini.
Je unanunua bidhaa au huduma unazouza au unazalisha mwenyewe?
Kuanzia sasa anza kuiona faida mapema tangu unaponunua au tengeneza bidhaa au huduma ya biashara yako kwa kutumia mbinu hizo hapo juu.
Kujifunza zaidi kuhusu jinsi unavyoweza kuianzisha biashara au kuikuza biashara uliyonayo hakikisha unajipatia kitabu chako cha UWEZO WA KUANZISHA NA KUKUZA BIASHARA.
Bahatika kupata nakala chache za ofa za kitabu hiki zilizobaki. Wasiliana nasi kupitia 0752 206 899. Karibu sana.
“Unastahili Zaidi Ya Unachokipata Sasa”
Karibu sana.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwl. & Kocha (Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;Simu 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz