Hivi Ndivyo Simba Anavyokufundisha Kupata Chochote Unachokitaka. Jifunze Sasa…


Categories :

Ungelinganisha kwa ukubwa wa umbo, simba amezidiwa na wanyama wengi tu. Lakini bado simba ni mfalme wa mwituni na anaweza kula mnyama yoyote yule.

Ungelinganisha kimo, simba ni mfupi kuliko wanyama wengi tu unaowafahamu. Lakini bado ana uwezo wa kula wanyama wote wafupi na warefu.

Kama ukilinganisha akili, kuna wanyama wajanja kuliko yeye. Lakini bado ana uwezo wa kufanikiwa kumakamata yoyote yule na kumla.

Nini kinachompa simba jeuli hii ya kumla mnyama yoyote yule anayemtaka?

Hii ndiyo sifa moja aliyonayo simba na ndiyo inayompa ushindi huu mkubwa katika maisha yake. Na wewe unaweza kuitumia kupata chochote unachokitaka maishani mwako.

Sifa hiyo ni MTAZAMO sahihi.  Hii ni picha anayokuwa nayo anapokutana na wanyama wengine.

[  ] Akimuona tembo haoni akiwa hatarini bali anaona akila kitoweo kizuri cha tembo.

[  ] Akimuona twiga haoni yeye akiwa chini sana akimchungulia kwa mbali sana. Bali huona akimla na ndiyo maana humuangusha bila kujali urefu wake na kupata kitoweo.

[  ] Hata kama faru watakuwa wamejikusanya wengi kiasi gani, simba humuona akila mmoja wao.  Ndiyo maana humchagua mmoja kisha kupambana na huyo mpaka mwisho.

Hii ndiyo sifa unayotakiwa kujikumbusha au kujifunza kutoka kwa simba ili kupata chochote unachotaka hata kwenye mazingira magumu.

[  ] Ili uweze kupata unachostahili, ona kuwa hakuna kitu chochote kinachoweza kukuzuia.

[  ] Licha ya fursa nyingi utakazokutana nazo, wewe komaa na moja kwanza mpaka upate matokeo.

[  ] Simba huona kabisa akifurahia minofu ya tembo. Na wewe ona ukiyafurahia matokeo ya mwisho hata kabla hujafika.

[  ] Kumbuka, hata kama yule mnyama aliyemshika atamburuza kiasi gani lakini atakuwa radhi, na hatamwachia mpaka amepata kitoweo. Usiache kufanya jambo lako la muhimu kwa sababu ya changamoto zitakazokukabili.

Ndugu! Una haki ya kufanikiwa maishani mwako.  Lakini unahitaji kuwa na mtazamo sahihi kama wa simba, jifunze kwake utaweza kupata chochote unachokitaka.

Ili kujifunza kiundani jinsi nguvu ya fikra inavyoweza kukufanikisha kupata chochote, hakikisha umekipata kitabu chako cha AMSHA UWEZO WAKO HALISI.  Kwenye kitabu hiki utajifunza jinsi ya kutengeneza picha kamili ya kitu unachokitaka, kuilinda na kubadili wazo hilo kuwa matokeo.

Kuna nakala chache za ofa ya Januari zimebaki.  Wahi nakala hizi sasa. Wasiliana nasi kupitia 0752 206 899. Karibu sana.

“Unastahili Zaidi Ya Unachokipata Sasa”

Karibu sana.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwl. & Kocha (Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;Simu 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *