Hiki Ndicho Cha Kubadili Ili Kupata Matokeo Ya Tofauti.


Categories :

“Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo” Mithali 23: 7a.

Kile ulichokiamini na kukifanya ndicho kilichokupa matokeo uliyonayo sasa.

Ulichokiamini na kukiweka kwenye matendo ndicho kilichoumbika ndani yako.

[  ] Huwezi ukaumba udhaifu ndani yako kisha ukapata uimara nje.

[  ] Huwezi ukaumba umasikini ndani kisha ukapata utajiri nje.

[  ] Huwezi ukaumba woga ndani kisha nje ukawa jasiri.

[  ] Huwezi ukaumba malalamiko ndani kisha ukwa na uwajibikaji nje.

[  ] Huwezi ukaumba uvivu ndani kisha ukawa na bidii nje.

[  ] Huwezi ukaumba chuki ndabi kisha ukawa na upendo nje

Kama matokeo unayopata sasa ya kipato, mahusiano, afya, kazi na kiroho yanakuudhi, basi njia pekee ya kuyabadili mambo hayo ni kubadili picha yako ya ndani.

Picha yako ya ndani ni MTAZAMO WAKO.

Kumbuka unachokiona ndani yako kimeumbwa kwa muda mrefu.  Hivyo unahitaji muda na jitihada mahususi kubadili picha yako.

Kubadili mtazamo wako.
[  ] Pata maarifa sahihi.

[  ] Zungukwa na watu sahihi.

[  ] Fikiri kwa usahihi.

[  ] Epuka mabishano yasiyo na tija.

[  ] Tuliza akili yako. Tahajudi & sali.

[  ] Pata muda wa pekeyako.

Naamini una mtazamo chanya juu ya nguvu ya maarifa sahihi kwenye mafanikio yako.  Kupata maarifa sahihi kupitia vitabu bonyeza kiunganishi hiki https://wa.me/message/Q6IVWM4M5LFTG1

Karibu sana.

“Unastahili Zaidi Ya Unachokipata Sasa”

Karibu sana.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwl. & Kocha (Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;Simu 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *