Hivi Ndivyo Umejihakikishia Kushindwa.


Categories :

Je na wewe umekuwa ukisema miongoni mwa kauli hizi?

[  ] Siwezi kufanya biashara na ukapata faida.

[  ] Mh mimi siyo wa kufanya mambo makubwa.

[  ] Huyu hawezi kuwa mteja…..naachana naye.

[  ] Hata nikimuambia atakataa….ngoja niache tu.

[  ] Siwezi kuanzisha biashara nikiwa kwenye ajira. Haitafanikiwa….

[  ] Hata nisipofanya leo nitafanya kesho

Hizi ni kauli ambazo umejiambia na kuziamini na kisha zikakuzuia kuchukua hatua. Na kwa sababu umekuwa huchukui hatua, hujapata matokeo uliyostahili.

Kama hujajaribu kitu, unapata wapi ujasiri wa kusema hakifanyi kazi?

Kama kuna watu wameshafanya na kupata matokeo unapata wapi woga wa kusema sitapata matokeo.

Kuanzia sasa acha kuhitimisha kuwa hakifanyi kazi kama hujakijaribu.

Pia usifanya mara chache na kuhitimisha kuwa hakifanya kazi.

Mr. Edison alijaribu mara zaidi ya elfu 10 kabla ya kufanikiwa kutengeneza taa ya umeme unayofurahia leo.

Wewe umejaribu mara ngapi kiasi cha kusema kitu ulichopanga kukifanya hakitoi matokeo?

Chukua hatua Leo.

  1. Anza kuchukua hatua za jambo ulilosita kulianzisha kwa muda mrefu sasa.
  2. Nenda kafufue jambo uliloliacha kwa kukosa matokeo baada ya kujaribu mara chache. Sasa kaa kwenye mchakato huo mpaka upate matokeo. “Unastahili Zaidi Ya Unachokipata Sasa”

Karibu sana.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwl. & Kocha (Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;Simu 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *