Itumie Siri Hii Ya Mkulima Kuanza Kutengeneza Uhuru Wako Wa Kifedha.
Je unatamani siku moja uepukane na tatizo la kipato kidogo kabisa?
Je unatamani siku ifike uwe na uhuru wa kifedha kiasi cha kufanya chochote halili bila kukwamishwa na ufinyu wa fedha?
Basi kuna siri moja anayo mkulima na unaweza kuitumia kufikia uhuru wako wa kifedha.
Mkulima mwerevu baada ya kuvuna mahindi yake, kwanza huchagua yale mahindi makubwa na ambayo hayajaharibiwa na wadudu kisha kuweka kama mbegu kwa ajili ya msimu ujao.
Huhifadhi vizuri mahindi hayo kiasi cha kutoyatumia hata kama kutakuwa na uhaba wa chakula.
Hivi ndivyo unavyotakiwa kufanya pale unapopata fedha zako. Kabla hujaanza kutumia basi toa kwanza mbegu kwa ajili ya baadaye.
Kwenye kila kipato unachokipata, weka nidhamu ya kutoa 10% na kuiweka kama mbegu.
Kazi ya mbegu za mahindi ni kuzalisha mahindi mengine. Kadhalika kazi ya mbegu ya fedha ni kuzalisha fedha nyingine.
Ndugu! Hakuna muujiza wa kufikia utajiri kama utatumia fedha yote unayoipata. Kumbuka kutoa mbegu.
Ili mbegu ya fedha iweze kuzalisha, basi weka sehemu ambayo inaweza kuzaa. Anzishia biashara, weka kwenye akaunti zinazokupa riba, wekeza kwenye hisa, wekeza kwenye vipande…..
Chukua hatua;
Anza leo. Kwenye kila kipato unachokipata hakikisha unatoa 10% kisha kuweka pembeni kama akiba. Weka akiba hiyo sehemu ambayo hutaweza kuichukua kirahisi.
Kama hutaweza kuanza na 10% basi anza hata na 5% au hata moja. Muhimu ni kuanza kutengeneza njia kuelekea uhuru wa kifedha.
By the way kitabu cha JENGA NIDHAMU KALI ni mwongozo muhimu sana kwako wa kujenga nidhamu kali ya fedha ikiwa na kutoa mbegu kwenye kila kipato chako ili kufikia uhuru wa kifedha.
Hakikisha unajipatia nakala yako leo ili uanze nidhamu hii muhimu ya kuepuka mtatizo ya kifedha maishani mwako.
Habari njema ni kuwa kuna nakala chache za ofa unazoweza kuzipata leo. Wasiliana nasi sasa kupitia 0752 206 899 kujipatia nakala yako.
“Unastahili Zaidi Ya Unachokipata Sasa”
Karibu sana.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwl. & Kocha (Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;Simu 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz