Vifahamu Vikwazo Vinne Vya Mafanikio Yako. Anza Kung’oa Kimoja Baada Ya Kingine Kufikia Mafanikio Unayostahili.


Categories :

1. Hofu ya kushindwa.

Waliofanikiwa walijaribu mara nyingi na kushindwa kabla hawajafanikiwa. Lakini kuna wengi walioshindwa ambao hawajajaribu kabisa au wamejaribu mara chache tu kwa sababu ya hofu ya kushindwa.
Ondoa hofu ya kushindwa kwani kujaribu, kushindwa kisha kurekebisha ndiyo njia ya kuyafikia mafanikio yako.

2. Uvivu.
Hujapata mafanikio unayoyataka kwa sababu hujaweka kazi kubwa.Hakuna mafanikio bila kazi. Kama unataka mafanikio makubwa lazima uweke kazi kubwa.

Kuna ujanja ambao huwa unatumia ili kuukuza uvivu wako, nao ni ‘siwezi’ kufanya hiki. Hakuna jitihada zozote baada ya kusema siwezi.

Ili kuanza kujenga nidhamu ya kazi sasa badala ya kusema siwezi jiulize nitafanyaje?

3. Tabia za kushindwa
Mafanikio hubebwa na tabia za mafanikio.  Kadhalika kushindwa hubebwa na tabia za kushindwa.

Tabia za kushindwa ni kama kutowajibika, kulalamika, uvivu, kutoweka akiba, kutoweka malengo, kutojifanyia tathmini.

Anza kujenga tabia za mafanikio:
[  ] Chukua jukumu la maisha yako kwa 100%.
[  ] Weka malengo kisha yaishi.
[  ] Penda kufanya  kazi kwa bidii.
[  ] Tenga angalau 10% ya kipato chako na wekeza.

4. Kiburi.
Ukijiona unajua kila kitu hutajipa nafasi ya kujifunza. Kujifunza na kutumia maarifa uliyojifunza kunakupa fursa ya kufanikiwa zaidi.

Usiruhusu kiburi kuchukua nafasi ya kujifunza.

Kuna nafasi ya kujifunza kisha kupata mafanikio zaidi ya uliyonayo sasa, nyenyekea utayafikia.

Je ni kikwazo gani kati ya hivi vinne kimekuwa kikikukwamisha sana kwenye safari yako ya mafanikio?

Anza kukiweka pembeni sasa ili kuanza kupata matokeo ya utofauti.

“Unastahili Zaidi Ya Unachokipata Sasa”

Karibu sana.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwl. & Kocha (Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;Simu 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *