Hii Ndiyo Hatua Unayotakiwa Kufikia Ili Kuweza Kupata Chochote Unachokitaka.


Categories :

Kama kusingekuwa na kikwazo chochote kile, ni kitu gani kikubwa ungetamani uwe nacho?

[  ] Je ni utajiri wa kiasi gani ungetamani uwe nao?

[  ] Je ungetamani uwe mtu wa namna gani kwenye jamiii(mahusiano)?

[  ] Je ungetamani kuwa na afya gani?

[  ] Ungetamani ufanye biashara gani?

Kuna hatua moja muhimu unayotakiwa ufikie ili uweze kupata chochote unachokita hapa duniani.

Hatua hiyo ni kwa wewe kujenga shauku kubwa sana juu ya kitu hicho.

Unahitaji kufikia hatua ambayo unajiona unakihitaji kitu hicho kuliko kitu kingine chochote.

Hii ni hatua ambayo unakuwa huna mbadala zaidi ya kukipata kitu hicho.

Kama kuna kitu ulikiona ni cha muhimu,  ukaanza kukifanya kisha ukaishia njiani, basi tambua kuwa hukufikia hatua hiyo.

Kama kuna sababu yoyote ile utairuhusu iwe kikwazo cha wewe kupata kile unachokitaka basi tambua kuwa bado hujajenga  shauku kubwa sana kukipata kitu hicho.

Na katika hali kama hiyo, bado unajiona una mbadala.

Shauku unayotakiwa kuijenga ni ile inayofananisha na shauku aliyonayo mtu anayetaka kufa maji. Katika mazingira kama hayo mtu hatahitaji chakula au fedha bali ni hewa kwa ajili ya kuokoa maisha yake.

Hii ndiyo siri ambayo watu waliofanikiwa huwa wanakuwa nayo.  Wanajitoa kupata matokeo bila kuruhusu sababu yoyote ile iwazuie kupata wanachokitaka.

Chukua hatua:

1.Chagua kitu kimoja kikubwa ambacho ndani yako kuna msukumo mkubwa wa kukipta.

2.Tafuta KWA NINI KUBWA ya kukipata kitu hicho ambayo itashinda sababu zote za kutokufanya hata pale utakapokutana na chngamoto.

  1. Andika kitu hicho kisha ainisha nini unaweza kuanza kufanya sasa.

Hata hivyo kitabu cha JENGA NIDHAMU KALI ni mwongozo kamili wa kukusaidia kuamsha nguvu kubwa ya kujisukuma kuchukua hatua ili kufikia malengo yako.

Jipatie nakala yako sasa ili usiendelee kupoteza muda wa kupata kile unachostahili.  Wasiliana nasi kupitia 0752 206 899 kujipatia nakala yako sasa.

“Unastahili Zaidi Ya Unachokipata Sasa”

Karibu sana.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwl. & Kocha (Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;Simu 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz
 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *