Ushindi Wako Unaanzia Hapa. Hutaenda Popote Kabla Hujavuka Hapa Kwanza….
Kuna hatua muhimu sana anayofikia mtoto inayofanya aweze kusimama, kutambaa, kutembea na baadaye kukimbia licha ya kushindwa na kuumia mara nyingi.
Kuna hatua muhimu sana waliofanikiwa waliifikia ndiyo maana wamefanya makubwa licha ya kushindwa mara nyingi.
Hatua hii muhimu inaanzia ndani yako. Huu ni ushindi unaotakiwa uupate kwanza ndani kabla watu hawajaona matokeo yako nje.
Huu ni ushindi unaotakiwa uujenge ndani ya akili yako. Ushindi huu ni IMANI YAKO KUWA UNAWEZA.
Henry Ford alisema ‘Whether you think you can, or you think you can’t–you’re right.’ Ikiwa na tafsiri kuwa Kama unafikiri unaweza, au huwezi….upo sahihi.
Kumbe kufanikiwa au kushindwa huchaguliwa na mtu mwenyewe.
Kumbuka pale utakaposema huwezi hakuna kitu cha ziada utakachokifanya…huu ni uchaguzi wa kushindwa.
Lakini pale utakaposema naweza, kuna swali akili yako itajiuliza, nitafanyaje?
Swali hili ni muhimu sana katika kuamsha nguvu kubwa uliyonayo ndani yako.
Hivyo kuna matokeo makubwa ya kukupa mafanikio umeyakosa, kwa sababu tu ya kujisemea huwezi.
Lakini kwa sababu bado upo hai, kuna nafasi ya kuanza kusema naweza kisha kuchukua hatua za kupata matokeo hayo.
Chukua Hatua;
- Kumbuka lengo moja kubwa uliloliacha kwa kuona huwezi kufanya.
- Jiambie ninaweza mara nyingi uwezavyo. Una nguvu kubwa bado imelala tu ndani yako.
- Jiulize unawezaje huku ukiandika majibu yako yote.
- Anza hata kwa hatua ndogo kati ya hizo kubwa unazotakiwa kuzichukua.
- Kila ukikutana na changamoto jiambie unaweza, chukua hatua, shindwa, jifunze kuwa bora zaidi kisha pata zaidi.
Kwa msaada zaidi juu ya kuamsha uwezo wako wa akili, mwili, roho na hisia uliolala tu ndani yako hakikisha umekipata kitabu cha AMSHA UWEZO WAKO HALISI.
Huu ni mwongozo wa kukusaidia kupiga hatua kubwa zaidi ya hizo ulizozifikia sasa. Ni bahati iliyoje, leo utakipata kitabu hiki kwa bei ya ofa.
Wahi ofa yako sasa. Wasiliana nasi sasa kupitia 0752 206 899.
“Unastahili Zaidi Ya Unachokipata Sasa”
Karibu sana.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwl. & Kocha (Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;Simu 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz