Huko Ndiko Fedha Zako Zilikojificha!
Rafiki! Kama umekuwa ukijiambia fedha ni ngumu, fedha adimu, vyuma vimekaza, hii ni dalili kuwa fedha haikufikii kirahisi .
Kuna muda umefikiri kuwa labda kuna fedha ambazo zimetorokea sayari nyingine ndiyo maana zimekuwa adimu kwako.
Ukweli ni kuwa hakuna fedha iliyoiacha dunia, fedha zote zipo hapahapa duniani.
Sehemu mojawapo fedha ilikojificha ni kwa watu. Dunia ina watu zaidi ya bilioni nane sasa, hawa ndio walioshikilia fedha zako.
Je watakuachiaje fedha walizoshikilia?
Njia ya rahisi ya mtu kukuachia fedha ni wewe kutatua changamoto/matatizo yake.
Je ni changamoto gani unaweza kuitatua na watu wakawa tayari kukulipa?
Kujua changamoto ambazo unaweza kuzitatua, anza na wewe mwenyewe, una matatizo gani ambayo unatakiwa uyatatue?
Matatizo uliyonayo wewe ,na wengine wanayo, ukiyatatua watakulipa.
Watu wana matatizo katika maeneo mengi ya maisha yao. Je wewe unaweza kutatua lipi?
[ ] Je afya?
[ ] Je kifedha?
[ ] Kibiashara?
[ ] Chakula?
[ ] Elimu?
[ ] Sanaa?
[ ] Mavazi?
[ ] Starehe?
[ ] Mahitaji muhimu nyumbani?
[ ] Usafiri?
Chagua tatizo moja ambalo linawatesa watu kisha anza kulitatua. Unaweza kuanza kwa udogo kisha kuendelea kuongeza thamani zaidi.
Nakukumbusha kuwa;
[ ] Kama hakuna kipato chochote unachokipata sasa basi hutoi thamani kwa watu wengine.
[ ] Kama unataka watu wakupe kipato kikubwa zaidi, basi ongeza thamani unayoitoa.
Nakutakia kila la kheri katika kuanza kutatua changamoto za watu ili wakupe fedha walizozikumbatia.
Karibu sana.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwl. & Kocha (Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;Simu 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz