95% Ya Mafanikio Yako Imejificha Hapa…..
Kama kuna siri kubwa inatafutwa hapa duniani, basi ni siri ya mafanikio. Hii ni siri ambayo umeitafuta kwa muda mrefu sasa bila mafanikio.
Ungeifahamu siri hii tangu siku nyingi ungekuwa umeshafika mbalia sana.
Lakini kuna methali ya kichina inasema muda wa kupanda mti wa kivuli ilikuwa miaka 20 iliyopita, lakini kama muda huo hukupanda basi muda mwingine mzuri ni sasa.
Hivyo nami nakwenda kukuambia siri ya mafanikio sasa, ili uanze kuitumia kisha kupata mafanikio.
95% ya mafanikio ambayo umeyatafuta kwa siku nyingi ipo yamejificha kwenye msimamo. Ndiyo MSIMAMO.
Msimamo ni kufanya kitu kimoja kwa kujirudia rudia bila kuacha mpaka upate matokeo unayoyataka.
Licha ya kuweka nguvu ili kupata mafanikio lakini hujafanikiwa kwa sababu umekuwa mtu wa kugusa na kuacha.
[ ] Ulianzisha biashara, ulipoona hupati faida ukiifunga hata kabla ya wateja wengi kujua unachouza.
[ ] Kila wakati umekuwa ukiacha kile ambacho unakifanya kisha kukimbilia kwenye fursa mpya.
[ ] Umekosa ustahimilivu, kila changamoto imekuwa ikikutoa kwenye reli.
[ ] Umekuwa ukiwekeza kwa muda mfupi kisha kuacha kwa sababu ya kutaka matunda ya uwekezaji ndani ya muda mfupi tu.
Matone ya mvua hujaza pipa kwa kuendelea kudondoka kwa msimamo kwenye pia hilo.
Lakini pia matone ya mvua yakiendelea kudondoka kwenye zege, hufanikiwa kuchimba shimo kwenye zege hilo.
Chukua Hatua:
Chagua kitu kimoja chenye fursa ya kukua hata kama utaanza kidogo kisha jitoe kukifanya hicho kwa msimamo bila kuacha.
[ ] Je biashara gani hiyo?
[ ] Je ni kujilipa wewe 10% ya kila kipato chako
[ ] Je ni kusoma vitabu kila siku?
[ ] Je ni kuwekeza kwa msimamo?
Kufanya kitu kwa msimamo kitakupa 95% ya mafanikio; akili inachangia 5% tu.
Karibu sana.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwl. & Kocha (Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;Simu 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz