Hivi Ndivyo Unavyoweza Kubadilika Kisha Kufanikiwa…
Mafanikio ni siri na wengi hawazifahamu ndiyo maana hawafanikiwi.
Je utajisikiaje kama leo nitakuambia siri moja kubwa ya kupata mafanikio maishani mwako? …naamini utajisikia vizuri…
Siri hii imeainishwa na nukuu ya John C. Maxwell inayosema “You’ll never change your life until you change something you do daily. The secret of your success is found in your daily routine”
Ikiwa na tafsiri kuwa hutabadili maisha yako mpaka pale utakapobadili kitu unachofanya kila siku. Siri ya mafanikio yako inapatikana kwenye vitu unavyofanya kila siku.
Kumbe mafanikio yako hayapo kwenye vitu vingi unavyojaribu kuvifanya na kuviacha
BALI
Mafanikio yapo yapo kwenye vitu unavyorudia kuvifanya kila siku. Vitu unavyovifanya kila siku hugeuka tabia.
Kama hujapata mafanikio ambayo ulitamani uyapate au ulikuwa unastahili basi ni kwa sababu ya vitu unavyovifanya kila siku.
KUKUMBUKA:
- Umekosa mafanikio kwa sababu vitu unavyovifanya kila siku si vya mafanikio.
AU umekosa mafanikio kwa sababu hufanyi vitu sahihi kwa msimamo.
- Utaanza kuyapata mafanikio kama utaanza kuvifanya vitu vya mafanikio kila siku.
Mafanikio ni 5% AKILI na 95% MSIMAMO. Na msimamo huja kwa kurudiarudia vitu.
Kumbe unaweza kubadili kushindwa kwako sasa kwa kuchagua kitu vitu vichache vya mafanikio kisha kuvifanya kila siku au mara kwa mara.
Kama unataka kufanikiwa, fanya yafuatayo;
[ ] Amka mapema kila siku
[ ] Soma vitabu kila siku
[ ] Yaandike malengo yako kila siku
[ ] Ipangilie siku yako kila siku
[ ] Fanya uliyopanga kila siku
[ ] Jilipe kwanza kwenye kila kipato
[ ] Jifunze kitu kipya kila siku
[ ] Boresha kile unachokifanya kila siku
[ ] Tafuta wateja wapya kila siku
[ ] Wasiliana na wateja wako kila wiki
[ ] Fanya tathmini ya maendeleo yako kila siku
Rafiki! Kama kweli unataka mafanikio kwenye maisha yako, anza kufanya mambo haya kila siku ndipo utakapoanza kuona miujiza kwenye maisha yako.
Haya hivyo kitabu cha JENGA NIDHAMU KALI ni mwongozo kamili wa kuamsha nguvu ya kujisukuma ili kuweza kufanya mambo hayo kisha kuanza kupata matokeo uliyoyakosa kwa muda mrefu.
Jipatie kitabu chako leo. Zimebaki nakala chache za ofa. Wahi bahati yako sasa, wasiliana nasi kupitia 0752 206 899.
Karibu sana.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwl. & Kocha (Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;Simu 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz