Hatua Tatu Muhimu Za Kufikia Uhuru Wa Kifedha.
Rafiki! Je ungependa siku moja uwe huru kifedha? Yaani;
[ ] Ule unachotaka
[ ] Ujenge nyumba ya ndoto yako
[ ] Uendeshe gari la ndoto yako
[ ] Utarii unakotaka
[ ] Ufanya kazi unayoipenda au usifanya kabisa
[ ] Upate muda wa kuwa karibu na familia yako
[ ] Uliishi kusudi la maisha yako.
Basi kama ungependa siku moja ufikie uhuru huo, kuna hatua tatu muhimu za kupitia. Kadri unavyoanza kuzipitia mapema ndivyo unavyojisogeza kwenye uhuru wa kifedha.
- KUWEKA AKIBA
[ ] Matumizi yako yasizidi kipato chako
[ ] Toa thamani zaidi kwa kufanya kazi ili kuongeza kipato chako
[ ] Kwenye kila kipato jilipe wewe mwenyewe kwanza (10%). Hii ni akiba kwa ajili ya uwekezaji. - KUWEKEZA
[ ] Weka akiba yako kwenye maeneo yanayoweza kuzalisha fedha hizo zaidi
[ ] Wekeza kwenye VIPANDE, HISA, HATI FUNGANI, ARDHI, MAJENGO, BIASHARA…. - JIPE MUDA
[ ] Uwekezaji unahitaji muda ili kukupa faida
[ ] Anza kuwekeza mapema
[ ] Wekeza kwa msimamo
[ ] Kila faida ya uwekezaji iwekeze tena
Kwa kufuata hatua hizi tatu kwa msimamo na ukubwa ndipo uwekezaji wako utaanza kukuzalishia fedha nyingi bila ya wewe kufanya kazi.
Fedha hizo zitakuwa nyingi kiasi cha kutosha kumudu gharama za mahitaji muhimu ya maisha yako lakini na anasa pia.
Chukua hatua leo.
- Weka kazi kubwa na sahihi kwenye kile unachokifanya ili kuongeza kipato chako.
- Kwenye kila kipato unachokipata hakikisha unatoa kwanza angalau 10% na kuweka pembeni kabla hujaanza matumizi(akiba).
3. Wekeza akiba yako eneo ambalo litazalisha zaidi(Nakushauri uanze kwenye vipande).
Nakutakia kila la kheri kwenye kuianza au kuiendeleza safari yako ya uhuru wa kifedha.
Karibu sana.
Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwl. & Kocha (Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;Simu 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz