Hiki Ndicho Kinachokuchelewesha Kupata Matokeo…..Usikubali tena..


Categories :

Je kuna matokeo ambayo umeyatamani maishani mwako lakini mpaka sasa bado hujayapata?

Je unashangaa muda unavyokimbia kwako bila kuwa na maisha uliyokuwa unayategemea?

Ulipanga kufanya mengi mwaka 2024 lakini ni mwezi wa nne sasa tangu mwaka uanze na huoni dalili zozote?

Kama unayapitia hayo hapo juu basi tambua kuwa kuna kitu kimekosekana kwako, usipofanyia kazi hilo hakuna kitakachotokea.

Kitu hicho muhimu kinachokosekana ni NGUVU YA KUANZA.

Gari hutumia nguvu kubwa kuwa na kuanza kutembea kuliko kuendelea kutembea.

Ndege hutumia nguvu kubwa kukimbia kwanza ardhini ndipo ianze kuruka.

Kuna mtihani mkubwa wa kuanza kitu.

Kama umekuwa ukipanga kisha kuahirisha, tambua ni kwa sababu ya ugumu wa kuamsha nguvu ya kuanza.

Kama umekuwa ukianza vitu kisha kuishia njiani basi tambua ni kwa sababu ugumu wa kukamilisha mwanzo wa safari.

Hivyo hata wewe unahitaji kujisukuma sana kuanza kuchukua hatua kuliko unavyofikiri .

Hutapata matokeo yoyote bila kuanza.

Chukua hatua hizi muhimu ili kuweza kuanza.

  1. Ainisha kitu kimoja au vichache ulivyo na shauku kubwa  kuvifanya.
  2. Ainisha sababu kubwa ya kwa nini ukifanye kiti hicho. Utakosa nini usipoanza au utapata nini kikubwa ukianza kufanya?
  3. Jisukume kuanza kuchukua hatua ya kwanza. Kama unataka kuanza biashara, anza hata kwa kununua bidhaa na kuanza kuuzia nyumbani.
  4. Ukianza, usirudi nyumba, kila unapotaka kukata tamaa, jikumbushe kuwa hiii ni hatua ambayo natakiwa kuendelea kujisukuma.

ANZA LEO ANZA SASA ANZA NA CHOCHOTE ULICHONACHO.

Karibu sana.

Imeandikwa na Alfred Mwanyika,
Mwl. & Kocha (Uwezo Wako Halisi & Mafanikio),
Mawasiliano;Simu 0752206899/0714301952
Barua pepe: alfred@amshauwezo.co.tz
Tovuti: www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *