Jifunze Kwa Tai Ufanikiwe Sana.
TABIA 5/7;
Tai jike humpima dume kabla ya kumkubalia.
[ ] Tai jike humpa mtihani tai dume kabla ya kusema ndiyo.
[ ] Mtihani huo huanza kwa tai jike kupanda juu sana mawinguni kisha kushuka chini kwa kasi. Dume hutakiwa kumfuata.
[ ] Kisha tai jike huchukua tawi na kupanda nalo juu sana na kuliachia. Tai dume hutakiwa kushuka kwa kasi kulidaka tawi hilo kabla halijadondoka na kumrudishia jike.
[ ] Jike huendelea na mchezo huo mara kadhaa.
[ ] Kama dume atafaulu mtihani huo, ndipo atamruhusu ampande.
[ ] Umekwamishwa mara ngapi kwa kuwaamini watu haraka kabla ya kuwapima?
[ ] Umelizwa mara ngapi kwa kuwapa watu fedha ambao uliwaamini bila ya kuwapima kikamilifu?
“Ili uweze kufikia mafanikio makubwa unahitaji watu wengine lakini sahihi. Ili ujue kama ni sahihi, wapime kwanza kwa kuwap mitihani ya kutosha”
Usikose Tabia ya 6/7 kesho.
Mwl. Alfred Mwanyika
AMSHA UWEZO
www.amshauwezo.co.tz