Jifunze Kwa Tai Ufanikiwe Sana.
TABIA 6/7;
Hutengeneza kiota chenye miiba ili kuwafunza watoto wao.
[ ] Tai hutengeneza kiota chao sehemu ya juu sana ya miti ambako maadui hawafiki kirahisi.
[ ] Kiota chao huanza na matawi makubwa chini, miiba, vimti vidogo, majani laini, manyoya kisha miiba pembeni.
[ ] Ndipo jike hutaga mayai kuatamia na kutotoa vifaranga.
[ ] Kadri vifaranga vinapoendelea kukua tai huvisogeza pembeni kwenye miba ili iwachome na mara nyingine kutoka damu. Hufanya hivyo mara kwa mara.
[ ] Wakifikia hatua ya kuweza kuruka, wazazi hutoa kabisa manyoya na majani laini kwenye kiota ili wakutane na miiba ambayo maumivu yake huwalazimisha kutoka kwenye kiota na kuanza kuruka.
[ ] Maisha ya mafanikio yana changamoto zenye maumivu, jifunze uvumilivu ili upite vipindi hivyo kwa mafanikio.
[ ] Wafundishe wanao kukua hata kwa maumivu. Dunia ina mapito yote; raha na taabu. Naye atakuwa imara atakapobaki pekeyake.
“Utafanikiwa kutoka kwenye mazoea kisha kupiga hatua kubwa zaidi kama utakubali kuvumilia maumivu unayostahili”
Usikose Tabia ya 7/7 kesho.
Mwl. Alfred Mwanyika
AMSHA UWEZO
www.amshauwezo.co.tz