Maeneo Matano(5) Muhimu Ya Kuwekeza Katika Maisha Yako.
1. MAARIFA: Lisha akili yako maarifa sahihi. Huu ni mwanzo wa kuchukua hatua sahihi. Soma vitabu, hudhuria semina, soma makala…
2. AFYA: Fanya mazoezi, kula vizuri kisha lala (wastani wa masaa 6).
3. KAZI: Weka kazi kubwa kwenye kile sahihi unachokipenda. Kazi ni rafiki wa kweli hatakusaliti, ukiambatana naye atakupa mafanikio.
4. HISA: Kuwa sehemu ya biashara kubwa bila ya wewe kufanya kazi. Ingiza fedha angali umelala. Ili kufikia uhuru wa kifedha nunua hisa zizalishe fedha nyingine bila ya wewe kufanya kazi.
5. MAJENGO NA ARDHI. Ardhi ni hazina. Thamani yake huongezeka bila ya kufanya chochote. Ardhi na majengo yataendelea kuwepo kwa muda mrefu sana…..
Uwekezaji gani umeshauanza? Kama umeanza basi ongeza kasi, kama bado basi Anza LEO anza SASA na anza na CHOCHOTE ulichonacho.
Karibu sana.
Mwl. Alfred Mwanyika
AMSHA UWEZO
www.amshauwezo.co.tz