Husogei Kwa Sababu Umefujifungia Kwenye Uraibu Huu….
Umesikia uraibu wa pombe, sigara au madawa ya kulevya kisha ukajipiga kifua kuwa wewe huko hupo.
[ ] Lakini kuna uraibu mmoja ambao umeujenga na ndiyo uliokukwamisha usipige hatua kwenye maisha yako.
[ ] Huo ndiyi uliokufanya uendelee kufanya mambo ya kawaida ambayo yamekufanya kuwa mtu wa kawaida tu.
[ ] Uraibu huo ndiyo unaokufanya kila mwaka unaweka malengo lakini hakuna hatua zozote za maana unazozichukua.
[ ] Huu ndiyo unaokufanya wewe kujiona huna bahati na kuna kuna watu waliopendelewa zaidi.
[ ] Huo ndiyo unaokufanya ukate tamaa katiki mengi mazuri uliyoyaona mbeleni.
Uraibu huo ni kung’ang’ania kwenye eneo huru ; ‘comfort zone’
[ ] Ili upate matokeo ya utofauti huna budi kufanya kwa utofauti na kwa ukubwa…ulipojaribu kufanya hivyo na kuhisi maumivu ukaacha na kurudi kufanya ulivyozoea.
[ ] Ulipojaribu kuamka mapema na ukaona kuna maumivu unayapata, ukaamua kurudi kwenye comfort zone yako ya kulala sana.
[ ] Ulipojaribu kufanya kazi kubwa zaidi na ukahisi maumivu, ukaamua kurudi kwenye comfort zone yako ya kufanya kwa uelegevu.
[ ] Ulijaribu kuanza kuweka akiba na uwekezaji kisha ukakosa fedha ya starehe, ukashindwa kutoka nje ya comfort zone ..ukaenda kuchukua ile akiba na kuitumia.
Hakuna miujiza utakayoifanya chini ya jua bila kutoka nje ya comfort zone yako.
Jiulize comfort zone (mazoea) gani yamekukwamisha maishani mwako?
Ili kutoka nje ya comfort zone yako hakikisha unakuwa na sababu kubwa(KWA NINI KUBWA) ya kufanya ulichopanga hata kama utakutana na maumivu yoyote yale.
Je KWA NINI KUBWA yako ni kipato chako duni kilichokufanya kuingia kwenye madeni mabaya yanayokuumiza?
Weke lengo kubwa sasa kisha, ainisha KWA NINI KUBWA na anza kujisukuma kuchukua hatua licha ya maumivu unayoyapata.
Hata hivyo kitabu cha JENGA NIDHAMU KALI ni mwongozo wa kukusaidia wewe kuweza kuchukua hatua za malengo yako hata pale unapokuwa hujisikii. Kanuni kubwa ya mwongozo huu ni TOA MATOKEO SIYO SABABU. Wasiliana nasi kupitia 0752 206 899 ili ujipatie kitabu chako na kuanza kutoa MATOKEO na siyo SABABU.
Karibu sana.
Mwl. Alfred Mwanyika
AMSHA UWEZO
www.amshauwezo.co.tz