Kama Unakithamini Kiandike!


Categories :

Kuna mawazo mengi ya thamani umeyapoteza kwa sababu hukuyaandika..

Umejaribu kujikumbusha…lakini hukumbuki…inakuuma….lakini ungeandika ungekumbuka kirahisi au ungeenda kufungua daftari/notebook yako kisha kujikumbusha.

Usiishie kufikiri tu ..andika.
[  ] Unapokiandika kitu unaiambia akili yako kuwa kitu hicho ni muhimu.
[  ] Unapoandika kitu hicho kinakuwa wazi(clear) zaidi.
[  ] Ukiandika utakumbuka.
[  ] Ukiandika utatathimini.
[  ] Ukiandika utarithisha kwa wengine.

Andika ndoto yako.
Andika malengo yako.
Andika mipango yako ya kila siku.
Andika tathmini za utekelezaji wako.
Andika makosa yako.
Andika ushindi wako.

Ukipata wazo mahala popote pale andika kisha baadaye lifikiri kwa kina.

Kuwa na kijitabu unachoweza kutembea nacho ili uandike kila unapopata wazo…..

Anza kujenga tabia ya kuandika….hakika utaanza kupata matokeo bora na makubwa zaidi…

Jipatie kitabu chako cha DONDOO 366 ZA MAISHA YA MAFANIKIO. Kina maarifa na hatua 366 ambapo kila siku utasoma DONDOO 1 na kuchukua hatua 1 kwa mwaka mzima bila kurudia….ukichukua hatua 366 hutabaki ulipo…utaenda mbali sana. Kupata nakala chache za ofa zilizobaki tafadhali wasiliana nasi kupitia 0752 206 899.

Anza LEO Anza SASA Anza na ULICHONACHO.

Karibu sana.

Mwl. Alfred Mwanyika
AMSHA UWEZO
www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *