Mambo Matano Ya Kuzingatia Ili Kupata Mafanikio Unayoyatamani…..


Categories :

Je kuna vitu umekuwa ukivitamani kwa siku nyingi vitokee maishani mwako lakini huvioni vikitokea?

Je umekuwa ukijiuliza nini ukifanye ili uanze kupata matokeo yatakayobadili maisha yako kisha kuleta furaha unayostahili?

Kuna mambo matano ya kuzingatia ili kuweza kupata unachostahili maishani mwako?

1. Jua nini unakitaka.
[  ] Wengi hawafahamu nini wanataka maishani mwano.
[  ] Wakiulizwa wanasema….nataka kufanikiwa!
[  ] Unataka nini na kiasi gani?
[  ] Weka wazi kabisa tena kwa kuandika nini hasa unataka kukipata. Kama ni fedha, ni kiasi gani na lini? Unataka kuwa nani na lini?

2. Kuwa unachokitaka kwanza.
[  ] Hakuna matokeo yataonekana nje kama ndani hayapo. Ujionavyo nafsini mwako ndiyo ulivyo.
[  ] Amini unaweza kupata ulichotaka kupata; una uwezo mkubwa umelala ndani yako ukiuamsha utaweza.
[  ] Andika lengo lako mara kwa mara.

3. Weka mpango.
[  ] Ligawe lengo lako kwenye vipande vidogo vidogo.
[  ] Tambua nini cha kufanya kila siku ili kufikia lengo lako kubwa.
[  ] Tambua ni mbinu gani utatumia kupata matokeo unayoyapata. Njia gani utatumia kuongeza kipato chako? Mbinu gani utatumia kuanza kuweka akiba….je ukipata fedha utatoa kwanza akiba kisha kuifungia gerezani kisha kuendelea na matumizi mengine?

4. Weka kazi tena kubwa.
[  ] Kuwa na malengo mazuri na mipango mizuri bila kazi ni bure kabisa.
[  ] Utapata matokeo kwa kuweka kazi tena kubwa kwenye kile unachotakiwa kufanya.
[  ] Ukipanga fanya hata kama hujisikii.
[  ] Kazi ni rafiki wa kweli, ambatana naye
[  ] Hakuna njia ya mkato ya kupata mafanikio,  penda kufanya kazi nayo itakulipa.

5. Vumilia
[  ] Matokeo yanaweza kuchelewa…vumilia.
[  ] Unaweza kupitia magumu… vumilia.
[  ] Unaweza ukachekwa….vumilia.
[  ] Kama upo kwenye uelekeo sahihi na ukaendelea kuweka kazi, matokeo ni suala la muda tu..

Unataka nini maishani mwako? Zingatia mambo haya matano kuanza au kuendelea kutengeneza njia ya kuyafikia mafanikio yako.

Hata hivyo kitabu cha MWONGOZO  WA KUTIMIZA MALENGO YAKO kitakusaidia kukuongoza kwenye kutengeneza uelekeo sahihi wa fikra, nguvu, muda, uzingativu ili kuweza kupata kile unachostahili. 
Habari njema ni kuwa utakipata kitabu hiki kwa bei ya ofa ya mwisho wa mwezi sh 3,000/. Usijionee kwa kukosa ofa hii.

Lipia sasa sh 3,000 kwenye mpesa 0752 206 899(Alfred Mwanyika). Utapokea kitabu chako ndani ya dak. 3. Fanya hivyo sasa kabla ofa hii haijaisha.

Karibu sana.

Mwl. Alfred Mwanyika
AMSHA UWEZO
www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *