F1: Je ungependa Uingize Fedha Angali Umelala?


Categories :

Huwezi kubeza umuhimu wa fedha katika maisha yako. Kama hutakubali kuwa fedha ni mambo yote, utakubaliana na mimi kuwa fedha ni mambo mengi.

Karibu kila kitu unachohitaji maishani mwako utahitaji fedha. Hata hewa unayosema unavuta bure kuna mazingira ukiwa unaumwa utahitaji uilipie hewa hiyo.

……Fedha ni jawabu la mambo yote(Muhubiri 19:10).

Kwa sababu ili upate fedha ni lazima utoe thamani ambayo wengine watakuwa radhi kukulipa fedha, watu imewalazimu kufanya kazi wasizozipenda, kufanya kazi mpaka wanaingia kaburini ili tu kupata fedha, …..

Kwa kuwa busy kutafuta fedha wamekosa muda hata wa kuwa karibu na wapendwa wao, kuitarii dunia, kuishi makusudi ya maisha yao……

Huu ni utumwa wa fedha….fedha imewalalazimisha wafanye nini….

Je ungependa wewe usiishi kwenye utumwa huu?…

Warren Buffett alisema “”Ikiwa hutapata njia ya kutengeneza pesa angali umelala, itakulazimu kufanya kazi hadi ufe”

Huwezi kutoka kwenye utumwa wa kifedha kama hutatafuta namna ya fedha kuzaliana bila ya wewe kufanya kazi moja kwa moja.

Hali ya wewe kuingiza fedha za kumudu gharama za mahitaji yako muhimu na hata anasa bila ya wewe kufanya kazi moja kwa moja huitwa uhuru wa kifedha.

Utajisikiaje kama siku itafika fedha za kukutosha zitakuwa zinaingia mfukoni mwako bila ya wewe kufanya kazi?……naamini utajisikia vizuri sana

Rafiki, uhuru huu unapatikana kwa wewe kufanya uwekezaji kwenye maeneo ambayo wewe hutahusika kufanya kazi moja kwa moja. Badala yake fedha itakuwa inahaingaika(inakutumikia) kukuzalishia fedha nyingine.

Maeneo ambayo unaweza kufanya uwekezaji ni;
1. Hisa
2. Mifuko ya mitaji ya pamoja(Vipande)
3. Hatifungani
4. Majengo/Ardhi
5. Biashara inayojiendesha nk

Anza kuwekeza sasa kila sehemu ya kipato chako kwenye maeneo haya; fedha hizo zitaanza kuzaliana kiasi kwamba kuna siku zitakuwa zinaingia nyingi mfukoni mwako na hata usipofanya kazi utamudu gharama za maisha yako…..utalala huku fedha zikiingia.

Habari njema ni kuwa kitabu cha SAFARI KUELEKEA UHURU WA KIFEDHA ni mwongozo wako wa kukusaidia kuujenga uhuru huu wa kifedha. Kinakuongoza hatua kwa hatua jinsi ya kugawa kipato chako(hata hicho kidogo) kisha kuwekeza kwenye maeneo tajwa hapo….kisha kufikia uhuru wa kifedha.

Usikubali kuitumikia fedha mpaka kufa. Fanya maamuzi sahihi sasa. Wasiliana nasi kupitia 0752 206 899 kupata mwongozo huu kisha kuanza kuwekeza bila kujali kipato kidogo ulichonacho.

Anza LEO Anza SASA Anza na CHOCHOTE Ulichonacho.

Karibu sana.

Alfred Mwanyika
Trainer,  Author and Entrepreneur
AMSHA UWEZO
www.amshauwezo.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *