Huyu Ndiye Mganga Namba Moja Anayeweza Kutuliza Fedha Zako Zisipeperuke.


Categories :

Je umekuwa ukitoa jasho jingi, unapata fedha lakini baada ya muda mfupi huzioni?

Je ukipata fedha akili yako haitulii mpaka pale utakapokuwa umemaliza kuzitumia?

Je unafanya biashara lakini licha ya mauzo makubwa unayopata lakini huioni faidi yoyote?

Je umekuwa ukiweka fedha kwenye kibubu, lakini licha ya kubomoa vibubu vingi…lakini huna fedha yoyote?

Kama haya yanakukuta basi tambua kuwa kuna chumaulete wa fedha zako na ni vema leo ukamfahamu.

Nasikitika kukuambia kuwa chumaulete namba moja wa fedha zako ni wewe mwenyewe,  ndiyo wewe mwenyewe!

Na bahati mbaya ni kuwa chumaulete huyu ataendelea kupeperusha fedha zako mpaka pale utakapompata mganga wa kumumaliza chumaulete huyu.

Habari njema ni kuwa mganga wa kumtuliza chumaulete huyu yupo na anaitwa NIDHAMU KALI YA FEDHA.

Pata picha umefanikiwa kujenga nidhamu kali ambayo inakuwezesha kupata kipato zaidi, kuthibiti matumizi yasiyo ya lazima, kuwekeza kisha fedha kuanza kukuzalishia fedha nyingine bila ya wewe kufanya kazi……naamini itakuwa hatua nzuri sana maishani mwako.

Kufanikiwa kujenga nidhamu kali ya fedha imejificha kwenye siri ya kufahamu KWA NINI kubwa  ya kujisukuma kutokutumia fedha zako vibaya.

Kutumia fedha vyema ni pamoja na kuweka akiba na kufanya uwekezaji kwenye kila kipato unachokipata.

Habari njema ni kuwa kitabu cha SAFARI KUELEKEA UHURU WA KIFEDHA ni mwongozo wa kukusaidia kujenga nidhamu kali ya fedha kisha kukuwezesha kuwekeza na kufikia uhuru wa kifedha.

Jipatie kitabu hiki leo kwa bei ya ofa ili uanze kujenga nidhamu hii muhimu uliyoishindwa kwa muda mrefu.  Wasiliana nasi kupitia 0752 206 899 ili kujipatia nakala yako.

Unastahili Zaidi Ya Unachokipata Sasa.

Karibu sana.

Alfred Mwanyika
Trainer,  Author and Entrepreneur
AMSHA UWEZO
www.amshauwezo.co.tz
0752 206 899.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *