Kama Hupati Matokeo, Hii Ndiyo Sababu ..


Categories :

“Muda wa kuatamia ukifika, kuku huacha karibu kila kitu kisha kuyafunika mayai muda wote mpaka pale vifaranga vitakapotoka huku akiamini kuwa akiyaacha mayai na kwenda kustarehe, atayaua”

Una malengo mazuri ambayo kila mtu anatamani kuwa nayo.

Lakini ni muda mrefu sasa tangu umeyaweka, matokeo yako wapi?

Kuna hatua muhimu ulitakiwa kuichukua ili kupata matunda ya malengo yako.

Hatua hii ni ya kuweka kazi juu ya malengo yako.

Na si kuweka kazi siku moja tu, bali kuweka kazi kubwa na mfululizo mpaka kupata matokeo.

Jifunze kwa kuku…muda wa kuatamia ukishafika huahirisha kila kitu kisha hufokasi kwenye kuatamia mayai mpaka pale atakapoviona vifaranga.

Sia kwamba huwa hatamani kwenda nje kula, kunywa na kustarehe…la hasha bali hufokasi kwenye kuyakumbatia mayai.

Kuku hutambua kuwa akiyaacha mayai hayo yapoe atakosa vifaranga.

Umekosa matokeo ya malengo yako kwa sababu umeweka nguvu kidogo tu kisha ukaacha kisha ukastarehe au kuanza kufanya mambo mengine.

[  ] Ulipokutana na ugumu ukakata tamaa.
[  ] Fursa mpya ilipojitokeza ukaona hiyo itakuwa rahisi kuliko ambacho ulishaanza kukifanyia kazi.
[  ] Matokeo yalipochelewa ukaacha kwa kuona malengo hayo hayafai.

Je ni malengo gani ulipaswa kuyakumbatia na kufanyia kazi mwaka 2024?

Yaatamie malengo yako mpaka upate matokeo. Usihangaike na kila fursa. Komaa  na jambo moja kwanza mpaka upate matokeo.

Hata hivyo kitabu cha MWONGOZO WA KUTIMIZA MALENGO YAKO ni msaada mkubwa wa kukuwezesha kuweka na kutimiza malengo katika maisha yako ili kupiga hatua.

Kina hatua 10 muhimu za kufuata ili kuweza kupata matokeo makubwa ambayo umeyakosa maishani mwako.

Habari njema ni kuwa leo unapata nakala yako kwa bei ya ofa, sh 3,000 tu badala ya sh 15,000. Usipitwe na ofa hii; lipia sh 3,000 kwenye mpesa 0752 206 899(Alfred Mwanyika). Utapokea kitabu chako ndani ya dak. 3.

Unastahili Zaidi Ya Unachokipata Sasa.

Karibu sana.

Alfred Mwanyika
Trainer,  Author and Entrepreneur
AMSHA UWEZO
www.amshauwezo.co.tz
0752 206 899.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *