Hili Ndilo Lililokukwamisha Sana…..
Umekuwa na matamanio mengi maishani mwako lakini matamanio hayo yamebaki kama mawazo tu.
[ ] Kuna biashara ya ndoto yako umekuwa ukiiwaza muda mrefu lakini mpaka sasa h uh hujafanya chochote.
[ ] Umetamani kuwa mtu fualani hapa duniani, lakini mpaka sasa wewe ni yuleyule wa zamani.
[ ] Ulitamani mpaka kufikia umri huu uwe umeshafanya uwekezaji fulani, lakini mpaka sasa huna uwekezaji wowote licha ya fedha nyingi kupita mikononi mwako.
[ ] Umekuwa ukiwa mipango mizuri ya kuongeza kipato chako, lakini mipango hiyo imebaki kwenye makaratasi tu.
[ ] Umepanga mara nyingi kuanza kuthibiti matumizi ya fedha zako ili kuanza kuweka akiba na uwekezaji lakini mpaka sasa upo kwenye madeni mabaya.
Sababu mojawapo iliyokukwamisha ni kujiona bado hujajiandaa.
Kila wakati unapopanga kuanza kufanya jambo unajiona bado hujajiandaa.
[ ] Ulipopanga kuanzisha biashara ukajiona kama bado mtaji hautoshi na maarifa yako hayatoshelezi.
[ ] Ulipanga kuanza kuweka akiba kisha kufanya uwekezaji ulijiona kama kipato chako bado ni kidogo.
[ ] Ulipopanga uanze kuamka mapema ili kuipangilia siku vizuri na kuianza mapema, usingizi ulikushinda na kujifariji kuwa utaanza kesho.
Rafiki! Hakuna siku itafika na utajiona kuwa sasa upo tayari..
Waliopiga hatua walijisukuma kuanza hata pale walipojiona kuwa hawapo tayari….kisha wakaendelea kuongeza vile vinavyohitajika huku wakiwa safarini.
Hata gari huwa inawaka na kuanza kwa kasi ndogo kisha dreva huendelea kuongeza kasi.
Rejea mipango yako kisha angalia ni nini unaweza kuanza kufanya….
[ ] Unataka kuanza biashara basi …anza na mtaji huo mdogo.
[ ] Unataka kuanza kuwekeza, anza hata kwa kiasi kidogo hicho unachokipata sasa.
[ ] Unataka kuanza kuamka mapema basi anza hata kuamka dakika 10 kabla ya muda uliozoea.
Hakuna maajabu yatakayotokea kwenye mipango yako kama hutaanza.
Anza Leo, Anza Sasa Anza na Kile Ulichonacho.
Je ungependa upate mwongozo wa kukusaidia kujenga nidhamu kali itakayokuwezesha kujisukuma kuchukua hatua za mipango yako iliyosuasua kwa muda mrefu?
Kama jibu ni ndiyo basi kitabu cha JENGA NIDHAMU KALI ni mwongozo pekee ambao umewasaidia wengi kutoka kwenye kuahirisha mambo kisha kuweka kazi na kuanza matokeo waliyoyatamani siku nyingi.
Ni zamu yako sasa. Wasiliana nasi kupitia 0752 206 899 kujipatia nakala yako.
Unastahili Zaidi Ya Unachokipata Sasa.
Karibu sana.
Alfred Mwanyika
Trainer, Author and Entrepreneur
AMSHA UWEZO
www.amshauwezo.co.tz
0752 206 899.