Mambo 5 Ya Kuzingatia ili Kujenga Biashara Yenye Mafanikio…
Categories :
Biashara yenye mafanikio haitokei kwa bahati mbaya, bali inajengwa.
Kuna vitu unatakiwa uvifanye ili uwe na biashara yanye mafanikio.
- Weka malengo.
Baada ya kuwa na maono ya wapi biashara yako inataka kufika, sasa weka malengo na mipango ili ikusaidie kukuza biashara yako na kufika huko mbali.
Weka malengo juu ya mauzo kwa siku, wateja wa kuwafikia, faida ya kutengeneza,… - Jenga nidhamu kali
Kila mtu anaweza kuweka malengo kwenye biashara, lakini ni wachache wanaofanyia kazi malengo hayo.
Wewe kuwa miongoni mwa watu watakaojisukuma kuchukua hatua kisha kupata matokeo. - Toa thamani
Watu wananunua kwa sababu kuna kitu watafaidika nacho. Kila wakati mfikirie mteja wako. Biashara yako inatatua tatizo gani. Kila wakati ongeza thamani ya kile unachouza(Huduma na bidhaa). - Tathmini
Ili kujiboresha, kila wakati jiulize umepata nini kwenye malengo ya siku, wiki, mwezi au mwaka uliyojiwekea? Rekebisha makosa unayofanya….biashara yako itaendelea kuwa bora zaidi. - Jitofautishe
Ushindani ni mkubwa sana kwenye biashara. Unachokifanya(uza) kinaweza kufanywa na mtu mwingine kirahisi. Tafuta upekee wako ambao utawavuta wateja kuikimbilia biashara yako.
Anza kufanyia kazi mambo haya 5 kwa msimamo. Hakika biashara yako itaanza kunawili.
Misingi hii ya kujenga biashara yenye mafanikio imeelezwa kiundani kwenye kwenye kitabu chako cha UWEZO WA KUANZISHA NA KUKUZA BIASHARA.
Je ungetamani kuanzisha biashara ya ndoto yako au kukuza biashara inayosuasua? Basi jipatie nakala yako leo. Wasiliana nasi kupitia 0752 206 899.
Unastahili Zaidi Ya Unachokipata Sasa.
Karibu sana.
Alfred Mwanyika
Trainer, Author and Entrepreneur
AMSHA UWEZO
www.amshauwezo.co.tz
0752 206 899.